Ujumbe kutoka Serikali ya Ujerumani ukiongozwa Mkurugenzi wa Serikali ya Ujerumani anayeshughulikia Masuala ya Bara la Afrika, Dkt. Stefan Oswald umewasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya ziara ya siku mbili ikiwa ni pamoja na kusaini mikataba ya kusaidia Uhifadhi.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya
Hifadhi hiyo, Dkt. Oswald
amepokelewa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary
Masanja (Mb).
Katika ziara hiyo ametembeleaVisitors Center na kupata maelezo kuhusu vivutio vinavyopatikana Serengeti, ikolojia na historia ya uhifadhi kabla na baada ya ukoloni.
Aidha, ametembelea Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ikona na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya uhifadhi wanayoifanya.
MWISHO

Comments
Post a Comment