Na. Kadala Komba, Dodoma
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa bei elekezi ya sh. 27,000 kwa wananchi wote wa Jiji
la Dodoma wanaohitaji kuunganishiwa umeme majumbani kuwawezesha wananchi
wote kupata huduma ya umeme kwa urahisi.
Waziri Dkt. Medard Kalemani |
Waziri Dkt. Kalemani ametoa bei elekezi hiyo jana mara baada ya kufanya
ziara katika kata ya Ntyuka jijini, Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya
miradi mitatu ya umeme ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO).
Alisema kufuatia ziara hiyo alibaini
wananchi wengi wa eneo hilo hawajapata huduma hiyo kutokana na bei walizokuwa
wakitozwa ambao husababisha kushindwa kumudu na ta kukwamisha nia ya
serikali ya kufikisha umeme kwa wananchi.
“Tuna mradi na TANESCO wanaendea na
zoezi la kuwapitishia umeme wananchi huu una gharama takribani bilioni 12
zinakuja Dodoma ndani ya miezi sita lakini mradi wa pili wa Desification amabo
wakandarasi wameshaanza bilioni 48 zinaingia Dodoma tuna uhakika hakuna mwana Dodoma atakayeachwa,” alisema.
Aidha, Waziri Dkt. Kalemani ameelekeza wakandarasi
kuhakikisha wanasambaza umeme kwenye maeneo yote waliyo elekezwa
kabla ya siki 14 na kuhakikisha hawaruki nyumba yOyote kwani lengo
la serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma hiyo
ndani ya miezi 12.
“Kukatika kwa umeme mtoe taarifa
ndugu zangu ni wapi umekatika mimi naletewa taarifa nashindwa kumtuma Meneja
aende wapi matokeo yake unakaa na tatizo mwezi mzima na niagize TANESCO muweke
madawati ya huduma kwa wateja walio mbali na huduma za tanesco umbali wa zaidi
ya kilometa 60 haiwezekani mwananzengo asafiri kilometa 200 kufuta umeme kwa
kulipa sh.27,000,” alieleza
Dkt. Kalemani.
Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde ameishukuru serikali
kwa namna ambavyo imeendelea kutatua changamoto za masuala ya
umeme pamoja na kutoa bei elekezi ambayo itakuwa rafiki kwa wananchi wote.
Mbunge Anthony Mavunde |
“Niishukuru sana Serikali yetu kwa
kuendelea kutatua kero zanishati kwa wananchi wake. Mheshimiwa Waziri leo tumetumia
Ntyuka kama kielelezo cha maeneo mengine mengi ya jiji la Dodoma,” alibainisha.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani, Abel Majengo amemshukuru
waziri kufika katika eneo hilo na kutoa maelekezo ambayo yatawasaidia Wananchi
Kupata umeme kwa haraka.
“Kama ulivyotoa maelekezo serikali
inafanya klazi na sasa tutawaambia wananchi tangu miaka yote kulikuwa
hakijaguswa na mradi wa umeme bei ilikuwa ni chagamoto watu wengi wamefanya
wiring kwa sababu umetoa maelekezo tutaelekea tu kwenye maelekezo hayo,” alieleza.
Comments
Post a Comment