SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU MASHULENI/YATENGA BILIONI 298 KWAAJILI YA MPANGO WA ELIMU BILA MALIPO
Na
Rhoda Simba,Dodoma.
KATIKA
kipindi cha mwaka 2020/2021 serikali imetenga Sh. Bilioni 298 kwaajili ya
mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi.
Hayo yamesemwa hii leo jijini hapa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Pili wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara (TAPSHA).
Amesema
katika kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora serikali
itaendelea kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni ili kukidhi haja ya
wanafunzi na walimu
“Serikali
iko makini kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha
nyingi kwa ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,vyumba vya
madarasa, Nyumba za walimu na mabweni,”alisema
Amesema mabadiliko makubwa yamefanyika kwenye sekta ya elimu ya msingi ambayo yamechochewa na mpango huu wa elimu bure na ujenzi wa miundombinu hivyo ni wajibu wa walimu kusimamia fedha hizo kufanya kazi iliyokusudiwa.
Katibu Mkuu huyo aliweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili kuboresha elimu ya msingi.
“Ni
jambo la kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi
wizi wa mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,.
Amesema
“hata ninyi mtakuwa mashahidi kuwa tatizo la udanganyifu wa mitihani bado lipo
na sereikali suala hili halitalifumbia macho kwani kwa kipindi pekee cha
mwaka jana jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa
udanganyifu,”alieleza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa elimu Tanzania kutoka TAMISEMI ,Julius Nestory
alitumia jukwaa hilo kuwataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili ya utumishi wa Umma huku akisisitiza kuwa Serikali hatamvumilia
mwalimu yeyote atakayekiuka agizo hilo.
Amesema
siku za hivi karibuni yameibuka matukio ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali
wasio waadilifu kusambaza nyaraka za serikali kwenye mitandao ya kijamii na
kusema jambo hilo ni kinyume na tarativu za utumishi wa umma.
Nestory
amesema walimu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii hivyo ni jukumu lao
kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
“Matumizi
ya mitandao ya kijamii hayaepukiki katika ulimwengu huu,lakini mnapswa kutumia
kwa uangalifu bila kuharibu taaluma yenu,” alisema.
Awali,
Mwenyekiti wa Umoja wa walimu hao(TAPSHA)Rehema Ramole alisema
mkutano huo utasaidia mafunzo mbalimbali ya uongozi, haki na wajibu wao
na kukabiliana na rushwa.
Mwenyekiti
huyo (TAPSHA) ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi Jeshini
Ubungo jijini Dar es Salaam alieleza kuwa wao kama wakuu wa shule wanao wajibu
wa kukumbushana na kukemea vitendo vya rushwa na kuendelea kuiunga mkono
serikali dhidi ya kukomesha vitendo vya rushwa na uvujaji mitihani
mashuleni.
“Tupo
pamoja na Serikali yetu katika kukuza elimu nchini,Kauli mbiu ya mwaka huu
ambayo ni uongozi na usimamizi makini wa elimu utaimarisha na kuiendeleza Tanzania
katika uchumi wa kati inaonyesha wazi ni kwa jinsi gani tupo tayari kupokea
maagizo yoyote yanayotolewa na serikali yenye lengo la kuinua elimu,”amesema.
Mwisho.
Comments
Post a Comment