UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA WAHAKIKISHIA WADAU UTAYARI SERIKALI AWAMU YA SITA KUPOKEA WATALII
Na. Mwandishi Wetu, UFARANSA
UBALOZI wa Tanzania nchini Ufaransa umefanya mkutano wa wadau wa utalii
Ubalozini kwa madhumuni ya kuwahakikishia wadau hao utayari wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuendelea kupokea Watalii hususan kwa wakati huu baada ya
dunia kukumbwa na janga la ugonjwa wa Corona ambao umeathiri sana sekta
ya utalii duniani kote.
![]() |
| Sehemu ya wadau wa utalii nchini Ufaransa wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Samuel Shelukindo wakati akielezea utayari wa Serikali ya Tanzania kupokea watalii |
Aidha, katika mkutano huo, uliofanyika Septemba 9,2021 Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo alifahamisha wadau hao kuhusu juhudi zinazofanywa naSamia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ameamua kufanya ziara iitwayo "Royal Tour"katika maeneo makubwa yenye vivutio nchini Tanzania.
Balozi Shelukindo aliwaeleza wadau kwamba jitihada hizo zinalenga kuitangaza Tanzania upya (Rebranding) na vivutio vyake vya utalii. Takriban wadau 60 walishiriki mkutano huo ambapo miongoni mwao ni makampuni makubwa yanayojihusisha na utalii (Tour Operators), Waandishi wa habari wanaotangaza utalii, Wafanyabiashara.
Wakati huo huo, Ubalozi unaratibu ziara ya kundi la Watalii 77 wanaotegemea kwenda Tanzania kuanzia tarehe 7 mpaka 12 Oktoba 2021 kutembelea maeneo mbalimbali.
MWISHO

Comments
Post a Comment