SERIKALI YAELEZA MIKAKATI YAKE KATIKA KUTANGAZA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI

Na. Mwandishi Wetu,


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili iweze kupata watalii wengi na kuongeza mapato.

 

Mhe. Mary Masanja

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Mhe. Martha Festo lililokuwa likihoji kuwa Serikali ina mpango gani wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Katavi, amesema serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa wa Katavi waliandaa mpango mkakati wa kukuza Utalii katika mkoa huo mwaka 2019 na umesaidia kwa kiwango kikubwa kuitangaza hifadhi hiyo.

Amesema Hifadhi hiyo imekuwa ikitangaza Vivutio vya Utalii kupitia Vyombo mbalimbali vya habari vya ndani ya nchi na nje ya nchi ikiwemo mitandao ya kijamii kwa kuwa ni miongoni mwa Hifadhi zenye viboko,simba na twiga weupe.

Kwa upande wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damasi Ndumbaro amesema serikali ina mpango mkakati wa kushirikiana na Halmashauri zote, Serikali za mitaa na Wilaya kuutangaza utalii ikiwemo kuwatumia wabunge kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Martha Festo Mariki ambapo amesema serikali kupitia wizara hiyo imeweka mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii nchini ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Katavi lengo ikiwa ni kuongeza idadi ya Watalii nchini.

 

 

 


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.