WIZARA YA MALIASILI NA UTALI YATOA WITO KWA WANACHI KUEPUKA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI

Na. Mwandishi wetu, TABORA

 

Serikali kupitia   Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa wito kwa wananchi kuepuka kuvamia maeneo ambayo yametengwa kwaajili ya hifadhi kwani husaidia kuongeza pato la Taifa kupitia wawekezaji ambao huwekeza katika maeno hayo.

 

Naibu Waziri, Mary Masanja

Wito huo unatolewa na Serikali baada ya baadhi ya wananchi wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora kuvamia eneo la hifadhi ya Isawima na kufanya shughuli zao kilimo hali ambayo husababisha kurudisha nyuma maendeleo ya hifadhi hiyo.

 

Akitatua mgogoro huo leo kwa wananchi hao, Marry Masanja amesema serikali inatambua umuhimu wa maeneo ambayo yamevamiwa kwani yapo maeneo ambayo yalikuwa yametengwa na Serikali kwaajili ya hifadhi lakini kutokana na ufinyu wa maeneo imepelekea watu kuvamia maeneo hayo.

 

Aidha, Marry amewaeleza wananchi hao faida ya kuwa na maeneo ya uhifadhi ikiwa ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji ili maji yaendelee kuwepo katika maeneo yao lakini pia kuongeza wawekezaji ambao husaidia kuongeza pato la Taifa na hatimaye wananchi kupata huduma mbalimbali za kijamii kama vile za Afya.

 

 ‘’kwanza kabisa tunahifadhi kwaajili ya kulinda nyazo vya maji, takini tunatarajia kuweka wawekezaji ambao watasaidia kuongeza pato la Serikali na hili pato la serikali ndilo ambalo linakuja kukujengea wewe vituo vya Afya,huduma za shule kama ambavyo mnaona sasa hivi watoto wote wanasoma elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne ,shida mliyo nayo hapa ni wapi mkafanye shughuli za kilimo na ufugaji maeneo ni mengi sana ambayo yapo’’ Marry Amesema.

 

Wakati huohuo ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya na kiongozi wa TAWA kuwaonesha wananchi hao maeneo ambayo siyo ya hifadhi ili waweze kuendesha shughuli zao kilimo.

 

“Ndugu zangu uhifadhi unapaswa kuheshimika na nina waomba sana muheshimu sheria, kanuni na taribu za nchi na sisi sote tunaendeshwa kwa sheria” Marry amesema.

 

Katika hatua nyingine Marry ameagiaza wananchi ambao wanatarajia kutoa mazo yao kuyatoa kwa utaratibu wa vibali ‘’tulishaanza kutoa hayo maelekezo na nadhani baadhi yenu wameshaanza kuyatoa tutaruhusu hayo mazao ambayo tayari yameshalimwa na yanaonekana kwamba yamefikia hatua ya kuvunwa na tusione tena mtu mwingine anakwenda kulima kule na ukita kwenda kulima kule chukua kibali’’ Marry Amesema

 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoani humo Dkt. Aloyce Kwezi amesema maelekezo yote ambayo Naibu Waziri ameyaagiza watayatekeleza kwakuhakikisha kuwa wanaepuka migorogoro ya mara kwa mara.

 

“Hawa wananchi unaona waona mbele yao Naibu Waziri mimi nilikuja kuwasikiliza kero zao na niliposikia kero zao nilikuja kuziwasilisha kwako na Waziri wako, ombi lao kubwa hapa ni mipaka ilikuwa haieleweki inaanzia wapi inaishia wapi na lakini kubwa zaidi kwenye ile mipaka ambayo imepita wananchi wakashindwa namna ya kuendesha shughuli zao hivyo wakalazamika kuingia katika maeneo ya hifadhi, ninaomba maneo ya mipaka ya Isawima yapitiwe vizuri’’ Dkt Kwezi Amesema.  

 

Dkt. Kwezi amesema kero kubwa ambayo walikuwa nayo wananchi hao ni mazao ambayo wameyalima kwenye maeneo ya hifadhi ‘’Naibu Waziri nakuomba wananchi hawa wapewe vibali waende wakavune mazao yao bila ya kuwa na usumbu wowote ule’’ Dkt. Kwezi amesema.

 

Mwisho

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.