WALIOHUSIKA KUHARIBU MIRADI WAREJESHWE KUJIBU TUHUMA: RC SENDIGA

Na. OMM Rukwa

 

Mkuu wa Mkoa Rukwa Queen Sendiga ameagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa kuchukua hatua za kuwarejesha watendaji na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuharibu miradi ya wananchi ili wajibu tuhuma zao.

 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabwe wakati wa mkutano wa hadhara jana na kuagiza watendaji na watumshi wa serikali wanaotuhumiwa kuharibu miradi ya wananchi warejeshwe kujibu tuhuma zao badala ya kuhamishwa

Kauli hiyo ameitoa jana (Jumatatu, Novemba 07, 2022) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kabwe wilaya ya Nkasi ambapo walilalamika kuwa Mtendaji amehamishwa baada ya kuharibu mradi wa zahanati.

 

Mkuu wa Mkoa huyo alitembelea zahanati ya kijiji cha Kabwe na kujionea hali ya kukwama kwa ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo linadaiwa kupatiwa vifaa vya mabati na saruji toka kwa wafadhili mwaka 202o lakini halijakamilika.

 

“Mtendaji wa Kata aliyekuwa hapa arejeshwe kuja kutoa majawabu ya tuhuma za kutokamilika zahanati ya kijiji cha Kabwe wakati vifaa vya ujenzi vilitolewa na wafadhili” alisema Sendiga.

 

Katika hatua nyingine Sendiga ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo na kwa wahusika watakaobainika hatua za kisheria zichukuliwe haraka.

 

Kwa upande wake Diwani Kata ya Kabwe Asante Lubisa alikiri kupokelewa kwa vifaa vya ujenzi wa zahanati hiyo toka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mwaka 2020 lakini kutokana na ramani iliyopangwa kubadilika mradi umeshindwa kukamilika hadi sasa.

 

Mkuu wa Mkoa huyo akiwa wilayani ya Nkasi alikagua kituo cha Afya Kasu, Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa madarasa sekondari ya Kabwe na bandari ya Kabwe ambapo alisema hatokubali kuona miradi ikisua sua.

 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akikagua bandari ya Kabwe jana alipotembea kuona utendaji kazi wake


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akikagua bandari ya Kabwe jana alipofanya ziara wilayani Nkasi kuangalia miradi ya sekata ya afya.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali na wa kwanza kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP Theopista Mallya

Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.