WADAU WA SEKTA YA MISITU WAFUNDWA KUSIMAMIA MISITU YA ASILI

 



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewaasa wadau wa misitu kote nchini washiriki kikamilifu katika usimamizi na utunzaji wa maeneo ya misitu ya vijiji ili kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.

 

Ameyasema hayo leo Novemba 15, 2022 wakati wa ufunguzi wa warsha ya 22 ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA)mkoani Morogoro.

 

"Kasimamieni misitu vizuri msigawe maeneo hovyo, mkaweke mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuzuia uvamizi kwenye maeneo ya hifadhi" Mhe. Masanja amesisitiza.

 

Aidha, amewataka viongozi wa MJUMITA wawaelimishe wananchi juu ya usimamizi wa misitu na umuhimu wa uhifadhi.

 

Katika hatua nyingine Mhe. Mary Masanja amewataka viongozi hao wakemee mila potofu ambazo zinamkandamiza mwanamke na kumnyima fursa za kushiriki kwenye uhifadhi wa misitu .

 

'Tuchukue hatua mara moja kuhakikisha jinsia inazingatiwa ili kulinda misitu yetu na kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wa Misitu hiyo" ameongeza.

 

Aidha, amesisitiza kuwa misitu ikisimamiwa vizuri ina uwezo mkubwa wa kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi, kutunza vyanzo vya maji, kuwa makazi ya wanyama hai na chanzo cha mapato kwa jamii hasa kwa kutekeleza shughuli za ufugaji nyuki.

 

Lengo la warsha hiyo ni kujenga uelewa wa pamoja wa dhana za ujumuishi wa wanawake na vijana katika uhifadhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, kubadilishana uzoefu wa namna ya kutekeleza dhana ya ushiriki wa jinsia kwenye uhifadhi wa misitu, kujadiliana kuhusu fursa na changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika uhifadhi na ushiriki katika mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.