TAKUKURU DODOMA: TUMEANZISHA UFUATILIAJI WA ZOEZI LA UGAWAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO ILI KUZUIA UDANGANYIFU
Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa
Dodoma imeanzisha ufutialiaji wa zoezi la ugawaji wa pembejeo za kilimo ili
kuzuia vitendo vya udanganyifu na ubadhirifu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi
ya watendaji na mawakala wa pembejeo.
Akiongea mkoani hapa Novemba 29,2022 Mkuu wa Taasisi hiyo Sosthenes
Kibwengo amesema huko nyuma zoezi hilo lilikuwa likikabiliwa na changamoto hizo
hali iliyopelekea baadhi ya watendaji hao kufunguliwa mashauri ya jinai
mahakamani kutokana na vitendo hivyo.
‘Tunawasihi wahusika wote katika mchakato huo kuzingatia
taratibu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kufuja
pembejeo .’’ amesema
Aidha, Kibwengo amesema wamekuwa wakishirikiana na halmashauri za mkoa wa Dodoma kuhakikisha ushuru na tozo zingine zinazokusanywa
kwa njia za mashine za Kieletroniki za POS zinawasilishwa benki kwa wakati.
‘’Ufuatiliaji huu umewezesha kuokoa fedha shilingi 75,524,700
zilizobaki mikononi mwa mawakala kwa muda mrefu kuwasilishwa benki.’’ ameongeza
Kuhusu chambuzi 10 za mifumo ya utendaji na utoaji huduma ili
kubaini mianya ya rushwa , amesema wamebaini mfumo wa malipo ya fedha taslimu
katika halmashauri ya wilaya ya Bahi taratibu za matumizi ya fedha taslimu
zinakiukwa kwa fedha kutolewa benki na kuhifadhiwa muda mrefu bila kutumika.
‘’Na hivyo kutengeneza mwanya wa ubadhirifu wa fedha hizo.
Yamebainika matumizi kinyume na makusudio ,fedha kutolewa benki ili kufanya
kazi ambazo tayari fedha zake zilishatolewa awali na malipo kufanyika bila
kuonyesha sababu uhalali wa malipo hayo.’’ amesema
Katika hatua nyingine Kibwengo amezungumzia kuhusu vitendo
vya rushwa ya ngono vinavyo fanyika katika maeneo mbalimbali nchini kuwa ni muhimu
kuvunja ukinya dhidi ya vitendo hvyo.
‘’Rushwa ya ngono ni tatizo linaloingia mpaka kwenye utu wa
mtu. Tuvunje ukimya tuachane na hii tabia yetu ya kuogopa kusema haya mambo. Haya mambo si ya kificho kiivyo
kwa sababu yanakuathiri wewe.’’
Hatahivyo, amesema wanatarajia kuweka nguvu katika kuelimisha
wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo vya rushwa .
Mwisho.
Comments
Post a Comment