Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekutana na wadau mbalimbali
ikiwamo wadau wa mifugo kwaajili ya
kujadiliana na kuwasilisha changamoto za kikodi pamoja na mapendekezo ya
kuboresha mazingira ya kibiashara yatakayo jadiliwa kwenye Bunge lijalo la
Bajeti 2023/2024.
Akiongea katika kikao kilicho wakutanisha wadau hao jana jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Mifugo Tixon
Nzunda amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanajenga mazingira bora ya
ufanyaji biashara na uwekezaji kwenye Sekta hiyo
‘’Tunajielekeza kufanya mabadiliko makubwa kuwezesha sekta
kuweza kubadilika. Moja ambalo ndio kubwa ni tija ili kusukuma sekta kufanya kazi
zake kitaalam kwa maana yakwamba hatuwezi kuzungumza tija kama hakuna
utaalam.’’ amesema Nzunda
Aidha, amesema mwelekeo wao ni kuifanya sekta hiyo inafanya kazi kibiashara ili kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zinakidhi viwango
vya kitaifa na kimataifa kwaajili ya kupata soko.
‘’Tusaidiane na wenzetu kuhakiksha masoko yanapatikana ya
ndani na nje. Ili kuweza kuongeza wigo
wa kukua kwa sekta yetu. Na katika hilo Serikali kwa mwaka huu wa fedha
imejithidi kuwekeza katika maeneo haya hasa kwa sekta ya nyama.'' ameongeza
Katika hatua nyingine amesema wamejipanga kuimarisha huduma za
utafiti ili kusukuma kazi zinazofanywa
na wadau ziweze kufanywa kutokana na utafiti uliofanyika.
''Ndio maana tumejikita kuimarisha taaasisi ya TARIRI iweze
kufanya kazi yake Kupata mbegu bora. Hapa
kuna changamoto nyingi tunajikita zaidi kuhakikisha tunapata mbegu bora za
malisho.'' amesema
Mwisho.
Comments
Post a Comment