Na WAF- DOM
SERIKALI
Kupitia Wizara ya afya inaelekea kukidhi kiu ya Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa
kupeleka kusoma jumla ya madaktari 12 watakaotoa huduma katika fani mbalimbali
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo Novemba 8, 2021
katika kikao cha bunge, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Nancy Hassan
Nyalusi Mbunge wa viti maalumu.
Amesema,
Katika kuongeza idadi ya madaktari bingwa, Wizara imepeleka kusoma jumla ya
madaktari kumi na mbili (12) kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa ambao
watasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akifafanua
hilo Dkt. Mollel amesema, madaktari hao ni pamoja na; madaktari wawili
wanasomea kinywa, sikio na koo, madaktari bingwa wa mifupa wawili, daktari wa
magonjwa ya dharura mmoja, madaktari bingwa wa Watoto wawili, madaktari bingwa
wa magonjwa ya ndani wawili, daktari bingwa wa meno mmoja, daktari bingwa wa
usingizi mmoja na daktari bingwa mbobezi wa masuala ya Watoto mmoja.
Aidha, Dkt.
Mollel amesema, hadi sasa Hospitali hiyo ina jumla ya madaktari bingwa kumi na
moja 11, madaktari bingwa wa afya ya akina mama na uzazi wanne, madaktari
bingwa wa upasuaji wawili, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani mmoja, daktari
bingwa wa Watoto wawili, daktari bingwa wa macho mmoja na daktari
bingwa wa mionzi mmoja.
Mwisho.
Comments
Post a Comment