Na. Rhoda Simba, Dodoma
SERIKALI
imeaanza mchakato wakuhakiki stahiki za watumishi walioondolewa kazini kwa kosa
la kughushi vyeti kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, siku ya Mei Mosi 2022.
Akitoa
ufafanuzi wa kile kilichofikiwa katika ulipaji wa stahiki hizo Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma CPA. Hosea
Kashimba alisema mfuko huo unatarajia kulipa watumishi hao elfu tisini 9,000 ambao
watatumia takribani shilingi Bilioni 20.
"Mchakato
umeanza tarehe 1 Novemba kama ilivoagizwa na Rais na sisi tayari
tumeanza kupokea nyaraka kutoka kwa waliokuwa waajili wa wafanyakazi hao, na tutakapo
jiridhisha tutalipa fedha hizo kwa wale wote wanaostahiki.
Na kuhusu
watumishi walifatiki na wanapaswa kurejeshewa michango yao wale walioandikwa
kwenye urithi wafanye utaratibu wa kupata fedha hizo kwa kufika katika Ofisi
walizokuwa wameajili watumishi waliofariki ili waweze kupatiwa utaratibu wa
namna ya kuapata fedha hizo," alisema.
Aidha, alieleza kuwa wakati
wa kuunganishwa mifuko kiasi kilichokuwa kinalipwa kama pensheni kwa mwezi kwa
wastaafu kilikuwa ni shilingi bilioni 34 lakini mpaka kufikia sasa wastani wa
kiasi cha shilingi bilioni 60 kinalipwa bila kukosa kwa wastaafu zaidi
za 150,000 Kila ifikapo tarehe 25 Kila mwezi.
Alisema mifuko
hufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye miradi ya
serikali,wakati wa kuunganishwa mifuko PSSSF ilirithi madeni ya serikali
yaliyohakikiwa yenye thamani ya shilingi bilioni 731.40 mpaka sasa kiasi cha shilingi bilioni 500
kimelipwa na Serikali.
"Pia
nirudie kuishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa kutambua deni la michango kabla
ya 1999 maarufu kama (pre 99 liability) ambalo ni shilingi Trilioni 4.60
kwa kutoa hati fungani maalum yenye thamani ya shilingi Trilioni
2.17, haya yote
yanaleta matumaini ya kuwa na Mfuko wenye ustahimikivu na endelevu kwa ustawi
wa wanachama," alisema.
MATARAJIO YA
BAADAE
Ni pamoja na
kuongeza vituo vya uhakiki katika Halmashauri mbalimbali na kuanzisha utaratibu
wa kujihakiki kwa simu janja, Kila taarifa ya wanachama iwe kwenye mfumo, usimamizi
Bora wa miradi ili kupata matarajio kusidiwa.
Na
kuhakikisha mifumo ya PSSSF inasomana na mifumo mingine kutoka taasisi nyingine
za umma ya watoa huduma,kurahisisha uandikishaji wanachama na uletaji wa madai
kupitia mtandao (online claim submission), utaratibu huo
utasaidia kutoa huduma kwa haraka na kupunguza matumizi ya karatasi, kubuni mifumo
mipya na salama ya TEHAMA kulingana na mahitaji ya Mfuko, kutumia
mifumo ya tehama asilimia 85 ikiwa malengo ni kutumia asilimia 100 ifikapo
2023, katika
shughuli za Mfuko hivyo kuboresha utoaji wa huduma.
Pia alisema kuwa Kwa
kipindi cha miaka 4 mfululizo Mfuko umekaguliwa na kupata
hati safi na kuibuka mahindi wa tuzo inayotolewa na NBAA kwa utunzaji bora wa
mahesabu ya mwaka 2019/20 katika sekta ya hifadhi ya jamii na bima.
"Mfuko
kupitia Idara ya Manunuzi umeendelea kufanya manunuzi Kwa mujibu wa
sheria kwa mwaka 2021 ulipata matokeo bora ya asilimia 94 na Mfuko unatambua
moja ya changamoto kubwa kwa jamii yetu ni uelewa mdogo kuhusu sekta ya hifadhi
ya jamii,
PSSSF
imejipanga vizuri kuendelea kutoa elimu kwa wanachama na watanzania wote ili
kuhakikisha sekta hii inafamika vyema ili kuendelea kutoa mchango katika uchumi
wa nchi yetu," alisema.
Mfuko wa
PSSSF ulianzishwa mwaka 2018 kupitia sheria ya Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa
watumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2018, Mfuko huu ni matokeo ya kuunganishwa kwa iliyokuwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF (1942), LAPF (1944), PPF (1978) na
PSPF (1999).
Mwisho
Comments
Post a Comment