Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yakabidhi Msaada kwa Watoto waliopo kwenye vizuizi vya kisheria.

 

Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania  Bw Sylvester Mwakitalu, amekabidhi  msaada wa magodoro, taulo za kike, mashuka, mafuta na sabuni kwa Mkuu wa gereza la mahabusu Segerea Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Hamisi Lissu.



Mkurugenzi Mwakitalu amesema msaada wa huo pamoja na vitu vingine umetolewa kwa ajili ya kuwahudumia watoto ambao wameshikiliwa kwenye vizuizi vya kisheria kutoka na na makosa mbalimbali waliyoyafanya.

Msaada huo uliwasilishwa baada ya kuupokea kutoka Shirika la Utangazaji (TBC) ambalo lilitoa msaada huo kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa mchango wa Shirika hilo katika kuisaidia jamii.

" Nashukuru wadau wote wanaoendelea kutuunga mkono katika mapambano dhidi ya uhalifu na leo asubuhi nimepokea msaada wa magodoro, mashuka, taulo za kike, sabuni na mafuta kutoka Menejiment ya Shirika la Utangazaji Nchini( TBC) kwa ajili ya kuwapelekea watoto waliopo vizuizini na waliokinzana na sheria" anasema Mkurugenzi Mwakitalu

" Tunalo kundi la kubwa la watoto ambao wanakaa kwenye Magereza na wazazi wao ( wanawake) ambao wanapatikana na hatia au wameshtakiwa kwa makosa ya jinai kwa sababu moja au nyingine anakosa dhamana na kwenda gerezani wakiwa na watoto wao na hawa ndio kundi kubwa ambalo lipo Katika Magereza yetu" anasema Mwakitalu.

Akimkabidhi msaada huo kwa DPP, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Moses Chitama, amesema msaada huo unalenga kurudisha fadhila kwa jamii, hivyo alitoa wito kwa jamii na wadau mbalimbili ikiwemo Sekta binafsi na mashirika ya Umma kuiga mfano kwa TBC wa kusaidia jamii.

Chitama amesema msaada huo wenye thamani ya Sh 5milioni umetolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) kwenda ofisi ya Taifa ya Mashtaka( NPS) kwa ajili ya kuupeleka gerezani kwa watoto wa wenye uhitaji maalumu.

Kwa upande wake, Mkuu wa jereza la Segerea, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Hamis Lissu, amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kutokana na watoto kuhitaji misaada mbalimbali ikiwemo magodoro na sabuni na vitu vingine.

" Msaada huu utaenda kutumika kama ulivyokusudiwa kwa walengwa, hivyo tunaomba wadau wengine waige mfano kama huu ulioonyeshwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Shirika la Utangazaji nchini kwa kuwa kuwajali wahitaji" amesema SSP Lissu.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.