MAADHIMISHO YA WIKI YA LISHE VIJIJINI YAFANYIKE – RC SENDIGA

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameelekeza halmashauri zote mkoani humo kuandaa maadhimisho ya wiki ya utoaji elimu ya lishe bora katika ngazi za vijiji ili kukabiliana na tatizo la udumavu.

 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kaiwasha moja kati ya pikipiki (12) alizozikabidhi leo kwa Maafisa Lishe wa Halmashauri za mkoa huo ili zikatumike kutoa elimu ya lishe bora na chanjo vijijini. Kushoto ni Afisa Lishe wa Manispaa ya Sumbawanga  Bw. Nassoro Chacharika aliyekabidhiwa pikipiki hiyo

Ametoa kauli hiyo leo (Novemba 04, 2022) mjini Sumbawanga wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki Kumi na Mbili (12) kwa maafisa lishe wa halmashauri zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la udumavu ambao kwa Rukwa upo asilimia 47.9 kwa takwimu za mwaka 2018.

 

Sendiga alibainisha kuwa maadhimisho hayo yakifanyika itakuwa jukwaa zuri la wataalam wa lishe kutoa elimu ya uandaaji vyakula bora na ulaji sahihi kwa kutumia vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira ya Rukwa kwa kuwa mkoa huo ni mzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula.

 

Akitoa taarifa ya vifaa hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isaack alisema jumla ya pikipiki Kumi na Mbili zimetolewa kwa Halmashauri za Kalambo (4), Sumbawanga Vijijini (3), Nkasi (3) na Manispaa ya Sumbawanga (2).

 

Dkt. Ibrahim alisema pikipiki hizo zitakwenda kufanya kazi ya elimu ya lishe, kuboresha utoaji chanjo na kufuatilia magonjwa ya milipuko vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kuhusu pikipiki (12) zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maafisa Lishe kwenye halmashauri za Rukwa leo mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki (12) kwa maafisa lishe wa halmashauri za Rukwa zitakatumika kutoa elimu ya kudhibiti udumavu vijijini


Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.