BODI YA WAHANDISI: TUTAHAKIKISHA TUNAWEKA MASLAHI YA UMMA MBELE

Na. Rhoda Simba, Dodoma

 

KATIKA kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini, Bodi ya Wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi wa sekta ikiwemo na kupambana na vitendo vya rushwa.

 

Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Bernad Kavishe

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Bernad Kavishe amesema Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili.

 

"Wahandisi pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na maslah yetu binafsi nyuma na ndio maana tunachukua kiapo kuapa kuweka maslahi ya Umma mbele.

 

"Bodi ipo mstari wa mbele katika kupambana na rushwa manake rushwa ni adui wa uhai siyo tu adui wa haki lakini malengo mahususi ya bodi ni kuimarisha na  kuhakikisha udhibiti wa kazi za wahandisi na taaluma ya wahandisi kwasababu uhandisi hauishii shuleni uhandisi ni tunahakikisha mpaka mtu  ana staafu" alisema Mhandisi Kavishe. 

 

Aidha, Mhandisi Kavishe alitoa wito kwa watu wenye miradi kuacha kutumia wahandisi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ili kuondokana na malalamiko pale wanapoharibiwa kazi zao.

 

"Kinyume cha sheria kabisa kupata huduma za kihandisi nje na watu ambao hawajadhibitishwa na bodi mbalimbali za kitaaluma, ile leseni tunayokabidhi ile ndio kielelezo ambacho serikali imeipitisha kwamba huyu mtu kapata elimu sahihi hawana mashaka nae na ujuzi wake upo hai" alisema Mhandisi Kavishe.

 

Nae Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara majengo na tayari imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na endapo miradi ikiharibiwa ERB inahusika.

 

"Kuna kazi kubwa inafanyika na miradi mingi ndani ya nchi yetu ambayo inategemea ushauri wa wahandisi hawa na nichukue nafasi hii kuwapongeza mpaka sasa nchi yetu imezalisha wahandisi zaidi ya elfu 33 na 26 wapo sokoni wanafanya kazi, ikumbukwe kuwa   tulipokuwa tunapata uhuru mwaka 1961 tulikua na wahandisi wawili tuu leo tunazungumzia hawa walio kazini na vijana bado wapo vyuoni wanasoma wanaendelea kuzalishwa" alisema Msigwa.

 

Mwisho

 


Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.