Na.
Prisca Maduhu, DODOMA
Ujenzi
wa darasa katika shule ya sekondari Lukundo umefika asilimia 30 ukiwa katika
hatua ya lenta ukilenga kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na pia
kuwapokea kidato cha kwanza mwaka 2023.
Hatua ya ujenzi wa darasa na chumba kidogo cha ofisi ya walimu |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa shule ya sekondari Lukundo, Mwl. Asifu Makonda wakati
akisimamia mradi wa ujenzi wa darasa moja na ofisi ndogo ya walimu ujenzi
unaotekelezwa katika Mtaa wa Mtakuja Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mwl.
Makonda alisema kuwa shule hiyo ilipokea kiasi cha shilingi 20,000,000 katika
utekelezaji wa mradi huo. Kiasi hicho cha fedha kilipokelewa tarehe 1-10-2022
na kuanza ujenzi rasmi tarehe 11-10-2022.
Aliendelea
kusema kuwa, fedha hizi zitatumika katika ujenzi wa darasa moja, ofisi ndogo ya
walimu na ununuzi wa vifaa vya ujenzi.
Mkuu
wa shule alisema kwamba mpaka sasa wametumia kiasi cha shilingi 8,000,000 na
kubakiwa na shilingi 12,000,000 kwenye akaunti. Ujenzi huo unahatua nane, ukiwa
katika hatua ya tatu ya utekelezaji wake kuelekea ufungaji wa lenta, sawa na asilimia
30 ya ujenzi, alielezea.
Alisema
kuwa kabla ya kuanza kutekeleza mradi huo aliunda kamati tatu ambazo ni kamati
ya ukaguzi na mapokezi, kamati ya ujenzi na kamati ya manunuzi. “Darasa hili
moja na ofisi ndogo ya walimu ni msaada mkubwa ambao tunaishukuru Serekali
kupitia Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mradi huu. katika shule yetu,
itasadia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuwapokea wanafunzi wa
kidato cha kwanza 2023 na kwa walimu itasadia kuongeza vyumba vya kujandaa ili
kuongeza uwajibikaji,” alisema Mwl. Makonda.
Ikumbukwe
kuwa shule ya sekondari Lukundo ilianzishwa mwaka 2007, mpaka sasa inawanafunzi
1,315 ambapo wasichana ni 744 na wavulana ni 571.
Mwisho
Comments
Post a Comment