Na. Prisca Maduhu, DODOMA
Shule
ya Sekondari Itega inatekeleza mradi wa ujenzi wa darasa na ofisi ndogo ya
walimu kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuwapokea
kidato cha kwanza mwaka 2023 ili kuimarisha ufanisi wa kazi na kupunguza msongamano
wa walimu katika ofisi moja.
Hatua ya ujenzi wa darasa na ofisi |
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa shule ya sekondari Itega, Mwl. Briton Bwatota wakati
akisimamia mradi wa ujenzi wa darasa moja na ofisi ndogo ya walimu katika shule
ya sekondari Itega iliyopo Kata ya Nkuhungu katika Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Mwl.
Bwatota alisema kuwa shule ya sekondari ya Itega ilipokea kiasi cha shilingi
20,000,000 katika utekelezaji wa mradi huo. Aliongeza kuwa kiasi hicho cha
fedha kilipokelewa tarehe 1-10-2022 na kuanza ujenzi rasmi tarehe 10-10-2022.
Aliendelea
kusema kuwa, fedha hizi zitatumika katika ujenzi wa darasa moja, ofisi ndogo ya
walimu, ununuzi wa vifaa vya ujenzi pia ununuzi wa samani za darasani ambazo ni
viti na meza.
Mkuu
huyo wa shule alisema kwamba kiasi cha shilingi 6,434,000 kimetumika na
kubakiwa na shilingi 13,566,000 kwenye akaunti. Ujenzi huo umefikia katika
hatua ya kuweka lenta ambapo ni sawa na asilimia 63% ya ujenzi huo, aliongeza.
Alisema
kuwa aliunda kamati tano kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.
Alizitaja kamati hizo kuwa ni kamati ya mapokezi, kamati ya ujenzi, kamati ya
manunuzi, kamati ya utekelezaji mradi na “tender bord”. Pia alisema kuwa walitoa matangazo ya kutafuta
fundi ujenzi, ambapo tangazo hili walilitoa katika ofisi ya kata na kubandika
matangazo, na baadae kuwapata mafundi na kuwafanyia usaili ili kumpata fundi
ambaye amekidhi vigezo.
“Mradi huu ni msaada mkubwa katika shule yetu, utasadia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kwa walimu utasadia kuongeza uwajibikaji,” alisema Mwl. Bwatota.
Ikumbukwe
kuwa shule ya sekondari Itega ilianzishwa mwaka 2007, mpaka sasa ina wanafunzi
771 ambapo wasichana ni 323 na wavulana ni 448.
Mwisho
Comments
Post a Comment