TSC YAWATAKA WALIMU KUENDELEA KUZINGATIA MIIKO NA MAADILI YA KAZI ZAO

 


Na Rhoda Simba,Dodoma 

 

ILI kuongeza tija ya ufundishaji Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)  imewataka walimu kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao na  kutekeleza majukumu kwa weledi  Ili  kuleta ubora wa elimu hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo  jijini hapa na Katibu Mkuu wa TSC Mwalimu Paulina Nkwama wakati akizungumza na waandishi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo.

Amesema,chombo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa walimu ili wafanye kazi yao kwa kuzingatia maadili huku akisema pamoja na jitihada hizo lakini bado kuna walimu ambao wamekuwa hawazingatii miiko na maadili ya kazi yao.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, amesema walimu wasiozingatia maadili ya kazi yao ,huilazimu TSC kuwafikisha kwenye mamlaka zao za nidhamu kwa mujibu wa kanuni kwa ajili ya kushughulikiwa kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili kuwanusuru watoto na kuwafanya wapate huduma iliyokusudiwa.

“Tume hii imejikita katika zaidi katika elimu kwa walimu ili kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu ambapo watendaji wa wilaya wamekuwa wakifika shuleni kutoa elimu kwa walimu kuhusu ajira na maendeleo ya walimu pamoja na maadili na kujiepusha na makosa ya kinidhamu kwa walimu.”amesema Mwalimu Nkwama

Pia, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwapongeza walimu kwa kazi kuwa wanayoifanya ya kutoa elimu kwa watoto hapa nchini huku akiwasihi kwamba TSC ipo pamoja nao kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao .

“Naomba nisisitize kuwa TSC ni chombo chenu kimeundwa kuwahudumia ,hakipo kwa ajili ya kuwafukuza kazi walimu la hasha ,bali kimeundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kuwahudumia walimu katika ajira zao ,maadli ya utumishi wao kwa kuhakikisha kwamba walimu wanafanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya maadili ya kazi ya ualimu na maendeleo yao katika utumishi wa umma"amesema Mwalimu Nkwama.

 Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.