SERIKALI YACHUKUA HATUA KUTEKELEZA MIRADI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI..

 


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kutekeleza miradi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti mkoani Songwe wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji.

Akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Khamis alisema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza miradi hiyo ikiwemo uchimbaji visima katika maeneo yenye ukame ili wananchi waweze kupata maji kwa ajili ya matumizi.

Alisema pia Serikali inatekeleza miradi ya kuwezesha upatikanaji wa majiko banifu ambayo yanasaidia kupunguza au kuondosha kabisa vitendo vya ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa sambamba na kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala.

Katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inaondokana na ukame ambao na zoezi la upandaji miti linaendelea kutekelezwa kwa kupanda miti milioni moja na nusu kwa kila halmashauri.

“Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeanzisha na inasimamia Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira, Kampeni ya Soma na Mti ambayo inahusisha wanafunzi wa shule na vyuo kupanda miti kwa lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabanchi,” alisema Mhe. Khamis.

 

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Itumba wilayani ileje alisisitiza wananchi kuendelea kupanda miti katika maeneo waliyoachiwa ili kutunza mazingira.

 

Naibu Waziri Chilo alisema kuwa miti mingi inaonekana imekatwa hali inayosababisha ukosefu wa mvua katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Tayari kamati ya mawaziri nane wa wizara za kisekta imeshatembelea mikoa kumi na tisa kati 26 kamati imeshapeleka mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri na inaendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.