Na Mwandishi Wetu,Dodoma .
Serikali imesema jumla ya Miradi 44 ya Barabara yenye kilomita 1,523 inaendelea na ujenzi nchi nzima ikigharimu kiasi shilingi trilioni 3.8 .
Hayo yamesemwa Oktoba 29,2022 na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kupitia vyombo vya habari.
Aidha, amesema miradi hiyo ,ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi ambayo inahusisha miradi inayo gharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa Kupitia Washirika mbalimbali mbalimbali wa Maendeleo.
"Mradi mkubwa wa ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Msalato unaojumuisha ujenzi wa njia ya kurukia ndege na majengo ya abiria unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 360." amesema
Pia, amesema Miradi ya barabara 62 iko katika hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
"Miradi ya EPC+ F Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS imeanza utekelezaji wa Miradi ya EPC + F yenye urefu wa kilometa 2,533km. Makampuni yaliyokuwa “shortlisted’ yamealikwa tarehe 22 Septemba, 2022 kuwasilisha zabuni." Ameongeza
Wakati huo huo, amesema jumla ya miradi 43 ya barabara yenye urefu wa kilometa 2,021.04 na gharama ya Shilingi Bilioni 9.6 ipo katika hatua mbali mbali za upembuzi yakinifu na usanifu.
"Miradi ya Ujenzi wa Barabara na Viwanja vya Ndege ambayo imesainiwa mikataba katika Mwaka wa Fedha 2021/22 (Julai 2021 hadi Mei 2022) Katika mwaka wa fedha 2021/22, kati ya Julai 2021 hadi Mei 2022, jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa Barabara na Viwanja vya Ndege inayogharimiwa moja kwa moja na fedha za ndani na mingine kugharimiwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo ilisainiwa. " amesema
Mwisho.
Comments
Post a Comment