Na Rhoda Simba, Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi Oktoba 31,2022 katika Viwanja vya Jamhuri Kushuhudia Uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyia Agosti 23 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Senyamule amesema ni vyema kushiriki kwenye uzinduzi huo kwani zoezi hilo ni la kihistoria na hufanyika kila baada ya miaka 10.
"Ni siku ya kipekee na hapa tuna siku moja kufika siku ya kutangaziwa matokeo na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Nitoe shime wana Dodoma mje Kwa wingi kuanzia saa 12 asubuhi hapa kwenye viwanja vya Jamhuri,'' amesema
"Leo saa 6 usiku tutakuwa na shamla shamla ya kupiga Fataki zikiashiria kuwa Dodoma tupo tayari kuletewa matokeo ya sensa ya watu na makazi hivyo tujitokeze Kwa wingi wana Dodoma" ameongeza Senyamule
Uzinduzi wa Matokeo hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Matokeo ya Sensa ya Sita 2022 Mipango Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu"
Mwisho
Comments
Post a Comment