RAIS SAMIA KUZINDUA MUONGOZO WA MATOKEO YA SENSA

 


Na Rhoda Simba Dodoma 

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Muongozo wa matumizi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi mara baada ya kutangaza matokeo ya Sensa ambayo imefanyika Agosti 23 mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema muongozo huo ni muhimu kwani matokeo hayo yakipatikana kinachofuata ni matumizi.

Amesema kuwa takwimu zitakazopatikana zitasaidia katika shughuli mbalimbali za kupanga mipango zikiwamo taasisi za Umma, binafisi hata wafanyabiashara huku akisema kwa upande wa serikali bila takwimu hizo haitapanga Mipango yake.

Waziri Simbachawene, ameongeza kuwa wanahitaji takwimu ili waweze kupanga mipango ya serikali zikiwamo huduma za kijamii kama maji, umeme, hospitali, masuala ya kilimo na nyinginezo.

"Kama ambavyo tumewatangazia hivi karibuni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imo katika maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 utakaofanyika katika uwanja wa Michezo wa Jamhuri hapa jijini Dodoma"

Katika uzinduzi huo kama mlivyoelezwa katika taarifa zetu mbalimbali, Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Simbachawene amesema, Sensa ya Watu na Makazi hufanyika mara moja kila baada ya miaka kumi na matokeo yake ndio yanayotumika katika kufanya maamuzi yote muhimu yanayohusu maendeleo ya nchi kwa kipindi cha miaka kumi hadi Sensa nyingine.

 "Hivyo, uzinduzi huu ni tukio moja muhimu katika historia ya maendeleo ya nchi hivyo ndio maana Serikali imeamua kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa wananchi wa makundi yote ili waweze kushiriki katika tukio hili la kihistoria,

"Matokeo haya ni muhimu sana kwa makundi yote katika jamii, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji na hasa kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani Serikali itaweza kupanga mipango yake kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kulingana na idadi, mahitaji na mazingira wanamoishi" Amesema Simbachawene 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar anaeshughulikia Sera Bunge,Uratibu, na Baraza la wawakilishi Hamza Hassan Juma amesema zoezi hilo lilienda vizuri kwa upande wa Zanzibar na taarifa zilizopatikana zitasaidia kujua idadi ya watu kujua kasi ya ukuaji kwa baadhi ya Mikoa .

" Takwimu hizi zitatusaidia sana na hasa Katika masuala ya utafiti wenzetu wanaofanya tafiti zitasaidia kujua wanatafiti kwa watu wangapi" amesema Hamza.

Tarehe 31 mwezi Oktoba Rais Samia Suluhu Hassan atatangaza matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi hapa jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Marais wastafu wa jamhuri ya Muunganio wa Tanzania huku hafla hiyo ikiambatana na burudani mbalimbali.

Mwisho.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.