MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AITAKA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUONGEZA UELEWA KWA WATANZANIA KUHUSU MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JUMUIYA YA KIMATAIFA
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman, ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika Mashariki
kuongeza uelewa kwa wataanzania kuwezesha kuyafahamu masuala mbali mbali muhimu
yanayoendelea katika jumuiya za Kimataifa na Kikanda.
Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar
alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Stergomena Tax alieyefika Ofisini kwa Makamu kujitambulisha baada ya uteuzi uliofanywa
hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan.
Mhe. Makamu amesema kwamba yapo masuala mengi na muhimu
yanayoendelea katika Jumuiya hizo ambayo watanzania wa kawaida pamoja na
viongozi wanapaswa kuyafahamu katika hatua za michakato hadi utekelezaji wake kwa
mafunufaa ya watanzania wote.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba kufanya hivyo pia ni muhimu
kwani kutasaidia wananchi na Viongozi nchini kuzifahamu fursa mbali mbali za
kiuchumi na kimaendeleo zilizopo katika ngazi ya kikanda na kimataifa ili
waweze kuzitumia kwa faida yao na taifa kwa jumla.
Mhe. Othman ametolea mfano wa Jumuiya ya Kimataifa inayoshughulikia
Haki Miliki za Wabunifu Duniani (WIPO), kwamba zipo fursa nyingi ambazo
kutokana na kukosekana uwelewa kwa wananchi fursa hizo hazitumiki ipasavyo na
pia kukosekana uwakilishi wa kuchangia masuala mbali mbali pale inapohitajika.
Akizungumzia suala la Balozi mbali mbali zilizoko katika
Kituo cha Kenya ambazo uwakilishi wao pia unafikia Tanzania, kuhakikisha kwamba
shughuli na huduma zao wanazotoa zikiwemo za watalii wainafikia Zanzibar ili
nchi kuweza kunufaikia kupitia kuwepo kwao Tanzania.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Stergomena Tax, amesema kwamba wizara hiyo itayafanyia kazi maelekezo
aliyopewa na kwamba suala laushirikishwaji wa wananchi katika kujenga uwelewa
litawekewa mpango maalumu katika utekelezaji wake.
Amefahamisha kwamba hatua hiyo ni muhimu katika kurahisisha
utekelezaji wa masuala mbali mbali yanayotokana na Jumuia za Kikatanda na
Kimataifa ambayo nchi imeridhia itifaki zake na pia kusainiwa na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekelezwa nchini.
Akizungumzia suala la mikutano ya mabalozi inayofanyika Tanzania
, Waziri Tax amesema kwamba wizara hiyo itahaikisha kuwepo kwa uwiano sawa kwa
pande mbili za muungano katika masuala mbali mbali yanayotekelezwa kupitia
itifaki za kibalozi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment