HOSPITAL YA BENJAMINI MKAPA YAOKOA FEDHA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 4.43 KWA WAGONJWA AMBAO WANGETIBIWA NJE YA NCHI

Na Rhoda Simba Dodoma

 

IMEELEZWA kuwa Hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanikiwa kupandikiza figo kwa watu 31 nakuokoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bil 2.3 huku ikitibu watu 715 ugonjwa wa moyo na kati yao 39 walibainika na matatizo ya moyo nakuwekewa vipandikizi na kati yao 8 wamepandikiziwa betri kwenye moyo.

Dkt. Alphonce Chandika


Hayo yameelezwa  Leo na Dkt. Alphonce Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa (BMH) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya hospitali hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2022/ 2023 amesema watoto 14 waliozaliwa na shida ya moyo wametibiwa huku watoto 10 wakifunguliwa vifua na kufanyiwa upasuaji.

 

“Uwepo wa maabara hii ni uwekezaji muhimu wa kuokoa maisha ya wananchi hususani hapa makao makuu ya nchi kwahiyo tuna wananchi wawili ambao walihudumiwa kwa dharula na wakaokolewa maisha yao kuna baadhi ya wagonjwa ambao mapigo yao huwa yanaenda taratibu na chini hivyo huwa tunawawekea betri ya kuongeza mapigo ya moyo na kupitia maabara hii huwa tumeweza kuhudumia watoto waliozaliwa na matatizo ya matundu ya moyo” amesema Dkt Chandika

 

Aidha Dkt Alphonce amesema Bilioni 1.28 zimeokolewa kwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa 58 wa nyonga kwakuwawekea vipandikizi kwa gharama ya shilingi milioni 12 badala yakutibiwa nje ya nchi kwakiasi cha shilingi milioni 35 kwa mgonjwa mmoja.

 

“ukiangakia kwa hawa wagonjwa 56 tumeweza kuokoa jumla ya shilingi Bilioni 1.28 za kitanzania ambapo pesa hizo zilitakiwa zikawatibie hawa watu nje ya nchi Amesema Dkt Chandikwa 

 

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema bmh imeanza kutoa mafunzo kwa wataalamu wa usingizi na ganzi na tayari wataalamu 127 wamehitimu huku akibainisha kuwa hospiltal hiyo inakwenda kuongeza wigo wa huduma kwakujenga jengo maalum kwaajili ya matibabu ya moyo, upasuaji wa mifupa na ubongo ili kuhakikisha hospital hiyo inakuwa ya pili ya taifa.

 

“Tunatarajia hizi huduma pia tuweze kujenga jingo kubwa kwaajili ya ya huduma za ugonjwa wa moyo maana ndio yanakuja kwa kasi tunatarajia mpaka elfu mbili ishirini na tano tuwe tumekamilika" amesema Dkt. Chandikwa 

 

Mwisho

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.