Na Rhoda Simba,Dodoma
IMEELEZWA kuwa ili mwili wa
binadamu upate virutubisho vyote muhimu mtu mmoja anatakiwa kwa wiki walau ale
kilo moja ya nyama kwani virutubisho vinavyopatikana kwenye nyama nyekundu
havipatikani kwenye mimea na kitaalamu mtu anapaswa kula nyama angalau kilo
hamsini kwa mwaka.
Akizungumza na waandishi wa
habari Leo Oktoba 28 kuhusu utekelezaji wa majukumu ya bodi ya nyama
Tanzania kwa mwaka wa fedha 2022-2023 msajili wa bodi hiyo Dkt. Daniel Mushi
amesema kuna watu wamekuwa wakisema nyama ni mbaya lakini uzuri au ubaya wa
kula nyama unatokana na kiasi cha nyama mtu anachokula na aina ya nyama
anayokula.
"Sisi kama Bodi ya nyama
tunalojukumu na mkakati wa kuwahamasisha watanzania wale nyama,niseme wazi apa
kuna mkanganyiko kidogo kunawatu wamesema nyama nimbaya lakini suala la nyama
kuwa mbaya au nzuri ni suala la kiasi Cha nyama unachokula na aina gani ya
nyama unakula,"amesema Dk Mushi
Aidha amesema kuwa endapo mtu
atakula nyama kwa kiwango kinachotakiwa mtu huyo atakua na afya kwani itasaidia
kuimarisha kinga ya mwili yakupambana na magonjwa nyemelezi na nguvu yakufanya
kazi hivyo itasaidia kuongeza uzalishaji.
"Kama mnavyo fahamu nyama
ndio njia rahisi ya kuondokana na utapia mlo,mtu anapowaambia watanzania wasile
nyama nadhani haelewi vizuri hali ilivyo katika ulaji wa nyama na sisi kama
Serikali tunaompango wa kuhamasisha watanzania wale nyama lakini ulaji nyama
uliosahihi,"amesema.
Katika hatua nyingine amesema
kuwa bodi itahakikisha inalinda afya ya mlaji kupitia udhibiti na ukaguzi
sambamba na kuhamasisha uzajishaji bora wa nyama ili kupata masoko nje ya nchi.
"Kwasasa mtanzania mmoja
anakula nyama takribani kilo 15 kwa mwaka kuanzia januari mpaka disemba lakini
tunapaswa kula nyama angalau kilo 50 kwa mwaka kwa wenzetu Ulaya wanakula mpaka
kilo 100 mtu mmoja kwa mwaka,
Sasa unapokuwa nyama kiasi
kinachotakiwa kwanza unakuwa na afya unakuwa na nguvu ya kufanya kazi na
uzalishaji unaongezeka lakini pia unakuwa na uwezo wa kinga ya mwili kuweza
kujikinga na magonjwa kinga zinakuwa Imara,"amesema.
Mwaka 2006 serikali ilitunga
sheria ya tasnia ya nyama sura ya 421 yenye lengo la kuwezesha mabadiliko
katika tasnia ya nyama, kuanzisha misingi thabiti ya usimamizi, kuhakikisha
upatikanaji wa bidhaa bora za nyama, kuendeleza ukuaji wa tasnia ya nyama na bodi
ya nyama tanzania ilianzishwa katika sheria hii ili kusimamia utekelezaji wa
sheria husika.
Comments
Post a Comment