Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Takwimu zinaonesha kwamba watu zaidi ya 60,000 hufariki kwa
kichaa cha mbwa duniani kila mwaka huku Kwa Tanzania, wastani wa matukio ya majeraha
kwa binadamu yanayotokana na kuumwa na mbwa ni 3,387 kila mwaka.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kichaa
cha mbwa duniani yaliyofanyika kitaifa kata ya Mpunguzi leo jijijini Dodoma, Mkuu wa
mkoa Rosemary Senyamule amesema Kwa mujibu wa ripoti ya WHO mwaka 2017, ugonjwa
wa kichaa cha mbwa husababisha wastani wa vifo vya binadamu 1,500 kila mwaka
nchini Tanzania.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule |
‘’Takwimu zaidi zinaonesha kuwa watoto chini ya umri wa miaka
15 ndiyo hupatwa zaidi na madhara haya kwa kuwa na ukaribu na urafiki na mbwa.’’ amesema Senyamule
Aidha, amesema kwa hapa Tanzania, kila mwaka kuna wastani wa
matukio 2,030 ya mbwa wanaodhaniwa kuwa na kichaa.
‘’Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Afya za Wanyama
Duniani (WOAH) and Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) kwa pamoja yamekubaliana
kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha mbwa ifikapo 2030. Njia ya kuu ya kufikia
malengo haya ya dunia ni chanjo kwa mbwa wote kila mwaka (annual massive
vaccination), kupunguza idadi ya mbwa, kuzingatia ufugaji bora wa mbwa ikiwa ni
pamoja na kufungia mbwa wasizurure mitaani.’’ameongeza Senyamule
Mbali na hilo, amesema Kwa Tanzania, ina Mkakati wa Kitaifa
wa Kutokomeza Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa wa mwaka 2019 (National Rabies Control
strategy, 2019).
‘’Lengo lake ni kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa na
hatimaye kuutokomeza kabisa ifikapo 2030. Pia, kuna Mpango Mkakati wa Afya Moja
(2015-2020) unaotoa wajibu wa kila mmoja katika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha
mbwa kwa njia ya chanjo.’’ amesisitiza Senyamule
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Prof. Hezron Nonga amesema watahakikisha mbwa wote wanachanjwa ili kuwakinga na
ugonjwa huo.
![]() |
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga |
‘’Natoa wiito kwa wananchi tuhakikishe kwamba tunachanja mbwa
wetu katika hii wiki lakini kwa muda wa mwaka mzima . Kwa sababu kalenda ya chanjo dhidi ya ugonjwa
wa kichaa cha mbwa ni kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa 12.’’
Perez Rumolwa aliyebahatika kuhudhuria katika maadhimisho ya
kilele hicho, amesema ugonjwa wa kichaa cha mbwa huweza kusababisha kifo ikiwa
mtu hatowahishwa hospitali huku akiishukuru Serikali kwa kutoa chanjo hizo .
Ndugu yangu mwenyewe, alikuwa binamu aling’atwa na mbwa
ikasababisha kifo chake.’’
Hapa nchini, kuna takribani mbwa milioni 4.5 na paka milioni
2 wanaofugwa kwa malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, kusaidia kuchunga
mifugo na uwindaji.
Mwisho.
Comments
Post a Comment