Na. Getruda Shomi, DODOMA
MHASIBU
wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Theresia Cosmass aeleza faida za ushuru wa
huduma kwa wananchi na wafanyabiashara kuwa ni kusaidia Halmashauri kupata
mapato yatakayotekeleza miradi ya kimaendeleo na kuimarisha huduma za kijamii.
Theresia Cosmass |
Alisema
hayo alipokuwa katika oparesheni ya kukusanya mapato katika Halmashauri ya Jiji
la Dodoma, kata ya Ihumwa Mtaa wa Flamingo, ikiwa ni siku ya pili ya oparesheni
hiyo.
Cosmass
alisema kuwa ushuru wa huduma ni muhimu kwani hupelekea maboresho ya
miundombinu na kuimarisha huduma za kijamii ambapo itasaidia wananchi kupata
huduma nzuri na kwa urahisi.
“kodi
ya ushuru wa huduma itasaidia kuboresha huduma za kijamii kama hospitali,
ujenzi wa barabara na kwa wafanyabiashara miundombinu ya barabara ambayo
itasaidia biashara zao kufikika kwa urahisi” alisema Cosmass.
Naye
Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Amri Kibwana aliongeza kuwa
mwitikio wa operesheni hiyo ni chanya na wafanyabiashra wanachukua hatua kama
inavyoelekeza sheria baada ya kupatiwa elimu.
“Pale
tunapokuta mapungufu, tunatoa elimu na kuwapa maelekezo namna ya kuanza
mchakato wa kulipa ushuru wa huduma na wafanyabiashara wanamwitikio mzuri wanakuja
ofisini kwaajili ya kufanya malipo” alisema Kibwana.
Akitoa
wito kwa wafanyabiashara wengine, Sospeter Kanichi amabae ni mfanyabiashara wa bucha
ya nyama alisema kuwa wafanyabiashara wafuate maelekezo kwa kulipa ushuru wa
huduma kwasababu ni njia majawapo ya kuchangia maendeleo ya nchi.
Sospeter Kanichi |
“Ni
sahihi kulipa ushuru wa huduma kwasababu tunachangia serikali yetu na
tunaboresha nchi yetu lakini pia biashara zetu. Hivyo, watu wasikimbie” alisema
Kanichi.
Oparesheni
hiyo iliyoanza jana itadumu kwa siku tatu na baadae itafanyika oparesheni
kwaajili ya kukagua utekelezaji.
MWISHO
Comments
Post a Comment