NIC YAWATAKA WANANCHI KUJIUNGA NA BIMA MBALIMBALI

 Na. Rhoda Simba, DODOMA

 

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limewaomba watanzania kujiunga na bima mbalimbali wanazozitoa huku likidai fedha zipo kwani katika kipindi cha miaka minne limeweza kuingiza shilingi bilioni 72.

 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, kwenye banda la NIC wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali Mkuu wa kitengo cha uhusiano kutoka Shirika hilo, Karim Meshack amesema NIC wamekuwa wakitoa huduma za bima za mali,ajali na maisha.

Amesema mwanzo shirika hilo lilikuwa haliwezi kujiendesha kibiashara  lakini kwa miaka minne mfuluilizo limekuwa likijiendesha kifaida.

Ametolea mfano kwa miaka minne mfululizo wameweza  kutengeza faida ya zaidi ya shilingi bilioni 72.

Amesema sababu ya kuingiza kiasi hicho cha fedha ni kutokana na kufanya mapinduzi katika maeneo matatu ambayo ni kwenye raslimali watu,ubunifu na kujiendesha kidigitali.

“Tulianza na rasiliamli watu kwa kutafuta wataalamu ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji ni kijana mwenye jicho la kibiashara.

Mwanzo Shirika lilikuwa linafanya kazi kama mashirika  mengine pamoja na kupata vijana wenye weledi wa kufanya biashara.

“Pia eneo lingine ni kwenye mifumo, Shirika linaendeshwa kwa mifumo ya kidigital sasa hivi hauwezi kukutana na karatasi shughuli zote zinafanyika katika system na tunafanya kazi kwa wateja kwa haraka.

“Sasa tuna mtandao mkubwa tupo katika kila eneo na unaweza kupata huduma ukiwa nyumbani umelala ukiwa nyumbnani kwako cha msingi uwe na hela.

“Eneo la tatu ni ubunifu mfano tuna mafao mengi ikiwa ni pamoja na kufiwa .Haina maana itaenda  kuchukua zile fedha na ukifika wakati wa kupata mafao unapata vilevile,” amesema Meshack.

Bw. Meshack, amewashauri watanzania  kwenda kwenye Shirika hilo kwa sababu watalipwa kwa wakati, shirika lina fedha za kutosha na anaweza kulipwa ndani ya siku 7.

Kuhusu kushiriki mkutano wa Mawakili Meshack alisema: “Tupo hapa hili ni Shirika la watanzania na lipo kwa ajili ya kusapoti jitihada za Serikali kwenye miradi ya  maendeleo ili Shirika lirudishe kwa jamii.

“Hawa mawakili ni wateja wetu na sio mawakili tu tunawashauri watu waje mfano Bima ya nyumba, nyumba ya milioni 100 ukiikatia bima unalipia 177 tu. Majanga hakuna mtu ambaye anayatabiri tunaitaji sapoiti ya watanzania,”amesema Bw. Meshack.

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.