Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Shirika la Bima la Taifa (NIC ) limesema kuwa limeweza
kutengeneza faida ya zaidi ya bilioni 73 katika kipindi cha mwaka 2020/2021 kutokana na watu kukata bima za mali,
ajali na maisha .
Hayo, yalielezwa Septemba 29, 2022 katika Mkutano wa Chama cha Mawakili wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano wa Shirika la hilo Karim Meshack alisema, Shirika mwanzo lilikuwa haliwezi kutengeneza faida, lilikuwa likiendeshwa kwa hasara.
‘’Lakini kwa miaka
minne mfululizo limekuwa likiendeshwa kwa faida. Na kwa mfano rekodi ya mwaka
2020/2021 tumeweza kutengeneza faida ya zaidi ya bilioni 73 . ‘’alisema
Aidha, alisema utengenezaji wa faida wa shirika hilo
imetokana na Shirika kufanya mapinduzi katika maeneo makubwa matatu ikiwemo
eneo la rasimali watu.
‘’Kwa maana tumetafuta wataalam wenye weledi wa kuweza
kuliendesha Shirika. Kwenye eneo hilo hilo la rasimali watu, ni pamoja na
kupata vijana wenye weledi wa kuweza kufanya biashara.’’ aliongeza
Akitaja eneo lingine , alisema ni eneo la kimfumo ambapo
Shirika limekuwa likiendeshwa kidigitali kwa maana ya mifumo ya tekinolojia ya
habari. ‘’ Sasa hivi ukija kwenye Shirika hauwezi kukutana na karatasi.
Shughuli zote za bima zinafanyika kwenye mfumo .’’ alisema
‘’Lakini, eneo la tatu ni la kiubunifu . Tumetengeneza upya
bidhaa zetu zote za kibima .Kwa hiyo tumekuwa na bidhaa nyingi ambazo zinajibu
changamoto za wateja wetu. Watu wanatakiwa kuja kutupa ushirikiano,kupata
huduma za bima .’’ alisisitiza
Shirika hilo, limewashauri watanzania mbalimbali kujitokeza
kulitumia kwani lina manufaa makubwa na litawasiadia kujikinga na majanga mbalimbali endapo yatatokea.
Mwisho.
Comments
Post a Comment