CHANDE: WADAU NA WATUMISHI MNAOHUSIKA NA UNUNUZI WA UMMA MZINGATIE SHERIA MSILIINGIZE TAIFA KWENYE HASARA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande, ametoa
wito kwa wadau wote na watumishi wanaohusika na ununuzi wa Umma kuzingatia sheria
na miongozo ili kutoingiza Taifa katika hasara.
Chande ameyasema hayo leo jijini Dodoma, wakati akipokea Ripoti
ya Tathmini ya Utendaji katika Ununuzi wa Umma PPRA mwaka 2021/2022.
‘’Tutaendelea kuchukua hatua kali kwa kadiri tunavyowabaini. katika
utendaji kazi katika ununuzi wa umma, kuzingatia mambo makuu manne ambayo kwenu
yatakuwa ni msingi wa utendaji bora katika ununuzi. Moja ni uwajibikaji ,mbili ni
uwazi, tatu utawala bora na thamani ya fedha.’’
Aidha, Naibu Waziri huyo ameipongeza PPRA kwa kuhakikisha kuwa
inafanya kazi zake kwa umakini na kufuata sheria na miongozo mbalimbali
inayotolewa na Serikali.
‘’Itakumbukwa, katika wasilisho langu la bajeti bungeni kwa Mwaka
wa Fedha 2022/23 nilitoa maelekezo kwa Wizara yangu kuhakikisha inasimamia mchakato
wa uboreshaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, kazi ambayo
nimetaarifiwa kuwa tayari imeshaanza na hivi karibuni wataweza kuwasilisha mapendekezo
kwa ajili ya hatua nyingine.’’
Katika hatua nyingine, amesema PPRA imekuwa na mchangao
mkubwa katika kusimamia ununuzi kwenye miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa
reli ya kisasa (SGR) na Mradi wa Kufua Umeme wa Mwalimu Nyerere (MNHPP).
‘’Nasikitika kuona bado baadhi ya taasisi hazikidhi matakwa
ya Sheria ya Ununuzi wa Umma hivyo kurudisha nyuma juhudi za kuleta maendeleo
zinazofanywa na Serikali. Nitakaa pamoja na viongozi wa wizara yangu na wa PPRA
ili kuona namna bora ya kushughulika na hizo taasisi zote zilizoshindwa kukidhi
matakwa ya sheria.’’
Sambamba na hayo amesema, kumekuwepo na ubadhirifu mkubwa wa fedha
za Umma wakati wa ununuzi kwa kutokuwa na weledi na uaminifu.
‘’Mathalani ukilinganisha bei ya bidhaa na huduma sokoni na
bei inayonunua Serikali zinatofautina kwa kiasi kikubwa sana. Fedha nyingi za
Serikali zinapoteza kwa mtindo huu.’’
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi ya PPRA
Dkt. Leonada Mwagike Licha ya uwepo wa mfumo huu wa ununuzi, zimeonekana changamoto
kadhaa kiasi cha kuifanya Serikali iamue kujenga mfumo mpya wa ununuzi.
‘’Changamoto hizo ni pamoja na Mfumo wa TANePS hauna uwezo wa
kulazimisha Taasisi nunuzi zinapofanya manunuzi kuchakata mpaka mwisho zabuni
zao ndani ya mfumo, Mfumo
kutokuwa na uwezo wa kujumuisha bei elekezi ili kudhibiti gharama za ununuzi na
kusaidia Serikali kupunguza gharama za ununuzi,’’
‘’Mfumo kutokuwa rafiki kwa watumiaji. Hii ni kutokana na mfumo
kuhitaji watumiaji wapandishe (upload) taarifa nyingi katika nakala ngumu.
Baadhi ya moduli kutokamilika
hadi kufikia Mwezi Julai 2022, Gharama za kuendesha mfumo na kufanya maboresho pale inapohitajika ni
kubwa na Kandarasi ya mfumo kufikia ukomo ifikapo mwezi Disemba
2023.’’
Ripoti hiyo , iliyowasilishwa inatoa tathmini ya utendaji kwa
kuelezea majukumu mbalimbali yaliyotekelezwa na Mamlaka katika Mwaka wa Fedha 2021/2222.
Majukumu hayo ni pamoja na
Kutoa huduma za ushauri katika ununuzi wa umma, Maelezo ya Mwenyekiti wa
Bodi ya PPRA, Kujenga uwezo kwa taasisi katika kutekeleza Sheria ya Ununuzi wa Umma,Kutekeleza
mfumo wa ununuzi kwa njia ya kielektroniki na Kusimamia Sheria ya Ununuzi wa
Umma.
Comments
Post a Comment