Na. mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George
Simbachawene amesema Mzee William Kusila alipenda kuona viongozi
wanazingatia miiko, na kuishi kwa kuwa mfano mwema kwa jamii.
![]() |
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mzee William Kusila katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Mtitaa-Bahi Mkoani Dodoma |
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na
Uratibu, Mhe. George
Simbachawene alipokuwa akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya
Mzee Williamu Jonathan Kusila aliyezaliwa Mwaka 28/02/1944 na kufariki
21/08/2022, iliyofanyika nyumba kwake kata ya Mtitaa-Bahi Dodoma 26/August/2022.
“Mzee kusila ni kipimo cha mtu muadilifu; mtu mwenye Upendo, na mtu
aliyefanya mambo mengi mazuri ambayo tunapaswa kuyaiga na kuyaenzi.”
Tumepoteza kiongozi wa kisiasa aliyeshika nafasi mbalimbali za umma na
kutimiza majukumu yake ipasavyo, ni mtu aliyepinga na kukataa rushwa, alisema
Waziri.
Aidha ametoa rai kwa Watoto wa Mzee Kusila kuzidi kushirikiana na
kushikamana ili kutunza jina na heshima ya baba.
“Amefafanua watu hawazaliwi sawa, mtatofautiana kwa uwezo wa elimu,
uwezo wa kipato na mambo mengine lakini wote ni Watoto wa mzee Kusila ni lazima
mtengeneze mamlaka itakayosaidia kuwaongoza kama familia”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema
Mzee William Kusila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Saba wa Dodoma kati ya Mwaka
(1993-1995) alikuwa Mbunge wa jimbo la Bahi na katika vipindi tofauti amekuwa
waziri wa kilimo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na amewahi kuwa Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Mzee William Kusila |
“Alifanya kazi kwa upendo Mkubwa; aliokuwa nao kwa wananchi wa
Dodoma, Baba yetu aliongoza kwa Vitendo na sio kwa kuagiza, kama alisema limeni
nayeye alikuwa analima”
Naye Mbunge Mstaafu wa jimbo la Chilowa Mhe. Hezekiah Chibulunje akitoa
salamu za rambirambi amesema anamkumbuka mzee Kusila kwa jitihada zake za
kuondoa Njaa Dodoma na kuhakikisha tunapanda mazao yanayostahimili ukame.
“Alikuwa na uchungu sana katika kuondoa njaa na vile vile katika swala
la zima la kusimamia elimu, nimefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana
bila nongwa”
Comments
Post a Comment