WAZIRI SIMBACHAWENE: KAZI NDIO HESHIMA YA MTU

 


Na Mwandishi wetu- Dodoma

Wakristo nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujietea maendeleo, changia pato la Taifa  na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wakfu Askofu wa  tatu wa Kanisa  la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma baada ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Askofu Donald Mtetemela kumaliza muda wake .

Waziri Simbachawene alisema chanamoto nyngi za kiuchumi katika jamii zitatauliwa endapo wananchi watajituma kufanya kazi na kuwa wabunifu   kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ambavyo maandiko matakatifu yanaagiza watu kufanya kazi.

“Lazima wakristo wa sasa tufanye kazi lazima tutae changamoto kwenye maeneo yetu maana imeandikwa katika biblia asiyefanya kazi na asile kwahiyo kufanya kazi ndio uhai wako, heshima yako na ukizalisha utaweza kuendesha maisha yako binfasi, utashiriki katika kazi ya Mungu na Taifa zima,” alisema Waziri Simbachawene.

Pia aliongeza kwamba serikalii itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo, kusimamia maadili na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watu wasiyo na hofu ya Mungu.

“Licha ya mchango mkubwa wa kanisa hili kwa serikali lakini kumekuwa na mmomonyoko wa maadili, magonjwa na majanga mbalimbali hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali ili kuokoa vijana na watoto wetu na ni matumaini yetu viongozi wa dini mkiendelea kusimama  imara  na kutoa huduma ya kiroho tutatatua changamoto hii,” alieleza.

Aidha alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea  kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa , ufisadi, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma pamoja na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo  Mndolwa aliipongeza serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuziunga mkono taasisi za dini  katika nyanja zote huku akimtaka Askofu Chiteto kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu hatimaye kufikia malengo ya kanisa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary  Senyamule  alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutumia fursa ya serikali  kushusha bei ya  mbolea kwa kujikita katika kilimo.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.