SERIKALI KUWEKA SERA ITAKAYOBORESHA UBUNIFU NCHINI.


Na Rhoda Simba Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa inatambua umuhimu wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo muhimu ya uchumi, na muhimili katika kuboresha maisha ya watu  nchini .

Aidha kwa kutambua hilo Serikali imesema kwamba inakwenda kuweka sera ambayo itaiongoza sekta hiyo ili kuboresha maisha ya wananchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo wakati akifungua mkutano wa wadau wenye lengo la kujadili na kutoa maoni juu ya rasmu ya sera ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu na kiunzi cha uratibu wa masuala ya ubunifu nchini.

Amesema maendeleo ya nchi mbalimbali duniani kote yanatokana na masuala ya yanayohusu Sayansi , Teknolojia  na ubunifu.

"Serikali kwakushirikiana na wadau mbalimbali wanaendelea kushirikiana na wadau katika kukuza uchumi ,jitihada hizo zitajumuisha kuandaa sera, kanuni na mikakati madhubuti ya kukidhi mahitaji ya nyanja mbalimbali za  kiuchumi,"amesema

Aidha Profesa Caroline ametoa rai kwa wadau wanaotoa maoni kwa njia ya mtandao,kuendelea kutumia fursa zilizowekwa ili nchi ipate sera ya sayansi na teknolojia na kiunzi kitakachojibu matarajio ya ubunifu.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Wizara ya Elimu anayeshughulikia  Sayansi Teknolojia na Ubunifu Profesa Maulilio Kipanyula amesema kikao hicho kinalenga kutoa fursa kwa wadau wa sayansi Teknolojia na Ubunifu nchini kujadili kutoa maoni kwenye rasmu ya sera ya sayansi na Teknolojia  inayotokana na sera ya ubunifu ya mwaka 1996.

Nae Muwakilishi mkazi kutoka Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu UNESCO Faith Shayo amesema mapitio hayo yatazingatia pamoja na masuala ya maazimio ya wananchi wanachama wa UNESCO kuhusu utafiti .

‘’ Shirika la Umoja wa Mataifa SIDA wanashirikiana na Wizara ya Elimu na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu UNESCO wanaendelea kutekeleza mradi unaolenga kuimarisha mambo yote yanayohusu elimu.’’

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Ubunifu (COSTECH) Dkt Amos Nungu amewataka  wadau hao kutumia vyema siku mbili hizo kuboresha sera hiyo.

 MWISHO

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.