Na. Rhoda Simba, DODOMA
KATIKA kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Dkt. Philp
Mpango, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.
Selemani Jafo ameagiza kuanzishwa kwa oparesheni kabambe yakuteketeza mifuko ya
plastiki katika maeneo mbalimbali nchini.
![]() |
Waziri Selemani Jafo |
Kadhalika amewaagiza wale wote ambao wamekuwa wakitumia vifungashio kama
vibebeo kuacha kufanya hivyo mara moja huku akizitaka kamati za ulinzi za Mikoa
na Wilaya kuchukua hatua kwa watakao kiuka.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo Agosti 26 jijini
hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya
mazingira amesema kampeni hiyo itatekelezwa katika maeneo ya maduka, sokoni,
magulio, mabucha ya nyama pamoja na samaki.
"Tukumbuke kwamba hivi karibuni tumeweza kukamata mizigo mbalimbali
katika maeneo
na kanda zetu
mbalimbali ambapo mizigo mingine imekuwa ikitokea nje ya nchi kwa kukamatwa
ikipita Katika mipaka yetu ya nchi,
"Jambo hili hali ridhishi hata kidogo kufuatia hilo Makamu wa
Rais wa Muungano na Mazingira Dkt.
Philip Isdor Mpango ameeleza kwamba kuanzishwe oparesheni kabambe ya
kuhakikisha kwamba hakutaonekana tena mifuko ya plastiki katika mitaa
yetu hili ni agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philp Isdor
Mpango" amesema Dkt. Jafo.
Aidha, ameagiza
wakuu wa Mikoa kupitia kamati za usalama kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa
pamoja na kudhibiti uingizwaji wa vibebeo hivyo mipakani sambamba na
kuwashirikisha viongozi wa masoko kama anavyoeleza.
"Nikiwa Waziri mwenye dhamana niagize maeneo yote watu wote
tutaenda kufanya kazi site kutekeleza agizo la Makamu wa Rais ambapo jambo la kwanza
tuwashirikishe viongozi wa masoko na viongozi wa magulio wao ndio shughuli hizo
za vifungashio vinatokea kwao" amesema Dkt. Jafo.
Agizo hilo linakuja kufuatia matumizi holela ya vifungashio ambapo
baadhi ya maeneo wazalishaji na wasambazaji wa vifungashio wamepeleka
vifungashio sokoni kutumika kama kibebeo swala ambalo ni kinyume na hivyo
kusababisha uchafuzi wa mazingira na kwenda kinyume na utekelezaji wa Sheria ya
mazingira nchini.
Mwisho
Comments
Post a Comment