![]() |
| Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (katikati) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique unaofanyika katika mji wa Victoria Falls, Zimbabwe |
Na Munir
Shemweta
Tanzania
imepiga hatua katika utoaji mikopo ya nyumba ambapo jumla ya mikopo 6,182
imetolewa hadi sasa ikilinganishwa na mikopo 579 iliyotolewa kufikia mwaka 2009
Aidha,
muda wa urejeshaji mikopo umeongezeka kutoka miaka 15 hadi 25 sambamba na riba
ya mkopo kupungua kutoka asilimia 20 - 22 mwaka 2009 hadi asilimia 15-19
zinazotozwa sasa.
Hayo
yalibainishwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula tarehe 27 Julai 2022 katika Mkutano Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter
Afrique unaoendelea kwenye Mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe ambapo
Tanzania inahudhuria kama mwanachama wa Taasisisi hiyo.
Akichangia
mada kuhusu jukumu la Benki Kuu kwenye soko la nyumba katika Bara la Afrika
huku akitoa uzoefu wa Taasisi ya ‘Tanzania Mortage Refinance Company’
iliyoanzishwa kufuatia utekelezaji wa mradi wa mikopo ya nyumba uliokuwa
ukisimamiwa na Benki Kuu, Dkt Mabula alisema kumekuwa na mafanikio
makubwa toka kuanzishwa taasisi hiyo ambapo kwa sasa jumla ya Benki na Taasisi
za fedha 33 zinatoa mikopo ya nyumba tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuanzishwa
kwa taasisi hiyo ambapo benki 3 tu ndizo zilizokuwa zikitoa mikopo.
‘’Kumekuwa
na mafanikio makubwa toka kuanzishwa Taasisi ya Tanzania Mortage Refinance
Company ambapo kwa sasa jumla ya benki na Taasisi za fedha 33 zinatoa mikopo ya
nyumba tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ambapo benki
3 tu ndizo zilizokuwa zikitoa mikopo’’ alisema Dkt Mabula
Hata
hivyo, Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwaeleza washiriki
wa mkutano huo umuhimu wa Benki Kuu kusimamia ipasavyo Benki na Taasisi
zinazotoa mikopo hiyo ili kuhakikisha zinatoa riba ambazo wananchi wataweza
kumudu kwa kuwa nazo zinawezeshwa kupata mitaji nafuu.
Akielezea
upungufu wa nyumba 3,000,000 na mahitaji ya nyumba 200,000 kwa kila mwaka
nchini Tanzania, Dkt Mabula alisema, endapo benki na taasisi za fedha
zitaendelea kuachiwa kutoza riba kubwa bila usimamizi haitafanikiwa kuwezesha
wananchi hususan wa kipato cha chini kumudu gharama za nyumba bora.
‘’Endapo
benki na taasisi za fedha zitaendelea kuachiwa kutoza riba kubwa bila usimamizi
haitafanikiwa kuwezesha wananchi hususan wa kipato cha chini kumudu gharama za
nyumba bora’’ alisema Dkt Mabula.
Mkutano
Mkuu wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique ulioanza Julai 25, 2022 unatarajiwa
kumalizika kesho Julai 29, 2022 na unahudhuriwa na nchi wanachama wa Bara la
Afrika ikiwemo Tanzania na umebeba kauli mbiu ya ‘Climate Change and the Built
Environment’.

Comments
Post a Comment