Na Rhoda Simba, Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amelipongeza Jeshi la Polisi kupitia kituo cha
afya Polisi Dodoma kwakujitoa kuhudumia wananchi kupitia kampeni ya afya bomba
pima .
Kampeni hiyo imeanza
leo hadi Julai 31 ambapo wananchi wanapata huduma ya kupima magonjwa
mbalimbali kama vile kisukari, figo, moyo, tezi dume, kinywa na meno pamoja na
magonjwa ya kina mama.
Akitoa pongezi hizo ,
Shekimweri amesema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 30 hiyo
ikiwa inaashiria uzalendo kwa manufaa ya umma yenye tija.
“Binafsi nmefurahishwa
na nimeridhishwa kwamba mmefanya kazi hii kizalendo askari mmetekeleza mradi
huu kizalendo. Askari mmetekeleza mradi huu kwa gharama nafuu mimi niwahakishie
kwamba tupo tayari kuwaaunga mkono katika ajenda hii kubwa muhimu kwasababu
mmeunga mkono jitihada za serikali katika kuwahudumia wananchi masuala ya
afya." amesema Shekimweri.
Ameongeza kuwa,
serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili yakuanza ujenzi wa
Hospitali ya Wilaya Nala jijini Dodoma huku akiwasisitiza wananchi kijitokeza
kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi.
“ Natoa rai kwa
wananchi jitokezeni kwa wingi moja kufanya shughuli za upimaji kwenye kituo cha
polisi hapa Dodoma na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetupatia million
500 za kuanza kujenga kituo cha afya Nala na muhimu Zaidi tujitokeze kuhesabiwa
ili mipango ya maendeleo ikapangwe vizuri’amesema Shekimweri ." ameongeza
Shekimweri
Akisoma risala mtoa
huduma wa kituo hicho Redemta Kisima ameelezea changamoto zinazokabili kituo
cha afya polisi Dodoma kuwa ni uhaba wa majengo hususani jengo la kujifungulia
wakina mama, madaktari bingwa na chumba cha upasuaji.
“Tunazochangamoto chache
zinazotukabili ikiwemo uhaba wa majengo hususani chumba cha kujifungulia, wodi
ya wagonjwa mahututi,wodi ya watoto ,wodi ya upasuaji, madaktari bingwa,
madaktari wa upasuaji na madaktari wa watoto wauguzi wafamasia na wataalam wa
maabara.” amesema Kisima
Mwisho
Comments
Post a Comment