Serikali yatangaza kuanza kwa mafunzo ya Makarani na Wasimaizi wa Sensa.


Na Rhoda Simba,Dodoma .

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa ametangaza kuanza kwa mafunzo kwa Makarani na Wasimamisi wa Sensa 20,5000 .

Dkt.Albina ameyasema hayo jana jijini Dodoma ambapo amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Julai 31 hadi Agosti 18 mwaka huu.

Amesema mchakato wa kuwapata watendaji hao wa muda ulienda vizuri na umefuata miongozo yote iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

“Baada ya kumalizika kwa mafunzo ya wakufunzi wa sensa sasa hatua inayofuata ni mafunzo kwa makarani na wasimamizi wa sensa ambao watafundishwa vizuri kuhusu kufanikisha tukio hili,na hapa nataka nisisitize kuwa kwa wasimamizi na makarani ambao watashindwa mitihani wataondolewa mapema na nafasi zao zitachukuliwa na watu wengine kwasababu tunayo hazina ya kutosha,"amesema Dkt. Albina

Amesema, kwa Makarani na Wasimamizi wa Sensa watakaofuzu mafunzo watakuwa na wajibu wa kufika katika maeneo ya kuhesabia watu siku mbili kabla ya zoezi la kuhesabu kuanza kwa ajili ya kutambua  mipaka ya eneo atakalofanyia kazi na kuhoji dodoso la kijamii huku akitoa rai kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaotoa siri za taarifa watakazo kusanya kutoka kwa wananchi.

Amesema, adhabu zipo kisheria na mkarani atakayetoa Siri za mtu atalipa faininya shilingi Milioni 2 au kifungo Cha miezi 6 au vyote kwa pamoja.

“Niwahakikishie wananchi kuwa taarifa watakazo zitoa zitakuwa salama kwasababu hawa makarani na wasimamizi kabla ya kupangiwa vituo watapewa kiapo cha utii ambapo atakayekiuka sheria itafuata mkondo wake.”amesema.

 MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.