MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI TRACKSUITS 120 WANAMICHEZO WA UMISSETA DODOMA MJINI


Na. Sifa Stanley, DODOMA

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi sare za michezo 120 kwa timu ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayojiandaa na mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Dodoma ili kuchochea hamasa kwa wanamichezo.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Sylas Sylivester (wa pili kushoto) akikabidhi tracksuit kwa Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma, Upendo Rweyemamu (mwenye miwani)



Sare hizo zilikabidhiwa kwa timu ya UMISSETA ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Sylas Sylivester katika hafla iliyofanyika shule ya sekondari Dodoma.

Sylivester alisema “mnamfahamu mbunge wenu ni mtu wa michezo, ameniagiza miwaletee vifaa vya michezo kulingana na idadi yenu. Nimewaletea ‘tracksuits’ 120. Sisi ni watoto wa mjini. Tuhakikishe tunachukua makombe yote, na ninaamini sura hizi zitatuletea ushindi. Mbunge wenu anawasalimia”.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Upendo Rweyemamu alimshukuru mbunge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wanafunzi hao. “Labda niwaambie wanangu mimi nimefanya kazi halmashauri nyingi, lakini ushirikiano nilioupata hapa sijawahi kuupata mahali pengine. Tangu nimefika hapa amekuwa akidhamini “tracksuits” hizi kila mwaka. Umwambie sisi tunamshukuru sana na hatutamuangusha tutahakikisha tunatafuta ushindi kwa ajili yake” alisema Rwenyemamu.

Nae mwanafunzi wa shule ya sekondari Bihawana, Bukuyu Bukuyu alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini kwa kuwaletea vifaa vya michezo na kuahidi ushindi. “Napenda kutanguliza shukrani zangu kwa mheshimiwa mbunge kwa kutuletea vifaa vya michezo hivyo tunaahidi makombe yote yatabaki mjini kulingana na walimu wetu walivyotufundisha. Tunamuomba mbunge wetu aendelee kuwa pamoja na sisi” alisema Bukuyu.

 

 



 

 

 

 

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.