Majaliwa: Serikali imetenga bilioni 10 kukarabati miundombinu ya michezo ....

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Serikali imetenga fedha shilingi bilioni 10 kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya michezo hususan viwanja ili kukidhi viwango na vigezo vya kuandaa mashindano mbalimbali ya ndani ya nchi, kikanda, kimataifa na kuwawezesha watanzania kutumia vizuri miundombinu hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika mbio za NBC Dodoma Marathon zilizo jumuisha washiriki zaidi ya 3,500 ambazo zimelenga kuchangisha fedha zitakazo tumika kuhudumia wanawawake wenye matatizo ya saratani ya shingo ya uzazi hapa nchini.

‘’Juhudi hizi za Benki ya NBC kupitia mpango huu wa NBC Dodoma Marathon zinaunga mkono juhudi za serikali zenye kulenga kuongeza ushiriki wa wadau katika kutoa michango yao kwaaajili ya sekta ya afya.’’ amesema Majaliwa

Aidha, amesema serikali itaendelea kusimamia uendelezaji wa michezo ili kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa.

‘’ Hakika Benki ya NBC ni taasisi ya fedha inayo tuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serikali yetu ya kuendeleza sekta ya afya lakini pia na michezo yenyewe.’’ ameongeza Majaliwa

Wakati huo huo Waziri Majaliwa , amewapongeza wadhamini wa mbio hizo wakiwemo Shirika la Bima la Taifa NIC kwa kuwa mstari wa mbele katika kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini.

Alexander Lajislaus kutoka Shirika la Bima ya Taifa NIC ambao wamedhamini mbio hizo , amesema lengo lao ni kuhamasisha wananchi  kufanya mazoezi  mara kwa mara ili kuweka miili yao sawa ambayo itawasaidia wananchi kuepuka kupata maradhi yanayo weza kuhatarisha maisha yao .

‘’ Tulivyo ona hiki kitu kinafanyikia Dodoma tukafurahi sana kwa sababu tutaitangaza Dodoma kwa kiasi kikubwa. Lakini pia kuwapa hamasa wananchi waweze kutembelea maeneo mbalimbali katika nchi hii Dodoma ikiwa ni moja wapo.’’ amesema Lajislaus

‘’NIC bado inaendelea kudhamini michezo kwa namna mbalimbali. Na Dodoma kiukweli imekuwa kati ya sehemu tumeona tuingie kwaajili ya kudhamini .Mwanzo huko nyumba hatukuwa tukifanya lakini tumekuwa tukishiriki katika marathoni nyingine.’’  ameongeza Lajislaus

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Theobald Sabi, amesema zaidi ya shilingi milioni 300 wameielekeza kwenye taasisi  ya saratani ya ocean road hivyo kuwezesha kufikiwa kwa wanawake zaidi ya elfu 9,000 waliopimwa saratani ya mlago wa uzazi.

‘’Kati ya hao wanawake 550 waligundulika kuwa na ugonjwa huu na hivi sasa wanaendelea na matibabu katika kituo hiki cha saratani ya ocean road . ‘’amesema Theobald

Naye,Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania  (RT}  Silas Isangi  amesema, kama nchi katika mbio za riadha imeanza kufanya vizuri  tofauti na ilivyo kuwa awali.

‘' Nipende kuwashukuru vijana wetu wanao shiriki mashindano haya ya riadha . Nchi yetu ya Tanzania katika riadha sasa imeanza kuchomoza. Na katika kumbukumbu zangu toka mwaka 2006 tulikuwa hatujawahi kupata medali lakini karibia miaka 16,17  lakini sasa safari hii mwenyezi Mungu ametubariki tumeanza kurudi katika ushindani.’’ amesema Silas   

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri, amesema kitendo kilicho fanywa na benki hiyo ni kuunga mkono ajenda ya serikali ya kufanya shughuli zake makao makuu ya nchi ‘

‘’Na mbio hizi zinaongeza hamasa ya michezo na kuitambulisha jiji letu la Dodoma kwenye ramani ya Dunia na kwenye ramani ya michezo.’’amesema Shekimweri 

Mwisho.

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.