Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera amesema uwepo wa Kampuni za gesi
za TOL Gases unakwenda kuongeza kasi ya uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya.
Mheshimiwa
Homera ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya Kampuni hiyo kuhusu uwekaji
wa mtambo mpya wa gesi ya carbon dioxide katika eneo la Ikama wilayani Rungwe.
kutoka katika Kampuni hiyo
Akizungumza
mbele ya wanahabari Ofisini kwake jijini Mbeya Homera ameitaja Kampuni ya TOL Gases
kuwa inaendelea kuongeza uchumi wa Mkoa na kwamba kiwango kikubwa cha gesi hiyo
kinapatikana ndani ya Mkoa wa Mbeya.
“Uwepo
wa Kampuni ya TOL Gases kwenye maonesho ya nanenane kitaifa Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini ndani ya viwanja cha John Mwakangale,imechagiza vizuri kuonesha
uwekezaji unavyopiga kasi mkoani Mbeya’’,alisema.
Hata
hivyo ametoa rai kwa kampuni ya TOL Gases na kampuni nyingine kushiriki katika maonesho ya nanenane mwaka
huu ili kuonesha uwekezaji mkubwa unaofanyika mkoani Mbeya.
Amesisitiza kuendelea kuongezeka kwa Kampuni kubwa mkoani Mbeya zikiwemo kampuni za
kukamua mafuta ya palachichi na kampuni kubwa za uvunaji wa gesi ya Carbon dioxide kwenye eneo
la Ikama wilaya ya Rungwe ni dalili njema ya Mkoa huo kusonga mbele.
Kampuni
ya TOL Gases iliyoanzishwa miaka Zaidi ya 70 inamilikiwa na watanzania wapatao
10,711 kupitia soko la Hisa la Dar es salaam na inajihusisha na uzalishaji wa gesi za
viwandani na hospitalini.
Kampuni
hiyo kupitia kiwanda chake cha carbon dioxide inahudumia viwanda mbalimbali
hapa nchini hivyo kuchochea ukuaji wa viwanda,hasa viwanda vya vinywaji baridi.
Kulingana
na taarifa ya kampuni hiyo,pia gesi hiyo inauzwa nchi za nje kama vile Congo
DRC,Zimbabwe,Zambia,Malawi na Burundi.
Kampuni
ya TOL Gases Julai 29 mwaka huu inatarajia kuweka mtambo mpya wa gesi ya carbon
dioxide katika eneo la Ikama wilayani Rungwe.
Mtambo
huo mpya utapoanza uzalishaji utaongeza kodi za serikali(Mrabaha),kodi ya
mapato, ushuru wa Halmashauri na kuongeza mauzo ya nje hivyo kuongeza fedha za
kigeni.
Imeandikwa
na Albano Midelo
Afisa
Habari,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Comments
Post a Comment