Na Munir
Shemweta
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula anahudhuria Mkutano
Mkuu wa Mwaka wa 41 wa Taasisis ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa
Victoria Falls Magharibi mwa Zimbabwe.
Tanzania
ni mwanachama wa Taasisi ya Shelter Afrique na inahudhuria mkutano huo kwa kuwa
ina haki ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya taasisi hiyo.
Shelter
Afrique ni Taasisi ya fedha inayoundwa na serikali za nchi za Afrika kwa
kushirikiana na Benki ya Afrika ambazo zinachangia mtaji kwa kununua hisa na
kujenga mtaji unaotumia na nchi wanachama katika shughuli za maendeleo ya
nyumba na miji kwenye Bara la Afrika.
Kauli
mbiu ya mkutano huo unaotarajiwa kumalizika tarehe 29 Julai 2022 ni ''Climate
Change and the Built Environment'' ambapo Tanzania kwenye mkutano huo
inawakilishwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa
Uendelezaji Milki Lucy Kabyemela.
Mkutano
mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique ni moja ya shughuli muhimu za
taasisi hiyo katika mikakati yake ya kipindi cha mwaka 2020- 2025.
.jpg)
Comments
Post a Comment