Na Nizar Mafita, KONDOA
Mtandao wa jinsia TNGP waibua kero katika vijiji vilivyomo kata ya Haubi wilayani
Kondoa
Miongoni
mwa kero zilizo ibuliwa na mtandao huo ni
ukosefu wa maji, uhaba wa Ardhi kwajili ya shughuli za kilimo na kero ya Tasaf
inayotolewa kwa kaya maskini
Kero hizo ibuliwa wilayani Kondoa katika mafunzo yanayoendelea ya
ukatili wa kinjinsia yanatolewa TNGP.
Akizungumza Anna Grace Rombiza amabye ni mtaalam
elekezi wa masuala ya jinsia amesema wamefika taika kata ya Haubi wilayani
Kondoa kwajili ya kutia elimu ya Ukatili wa kinjinsia ili jamii iweze kufahamu
vyema aina zote za
Ukatili wa kinjinsia na kuweza kukabiliana nazo pindi vitendo vya Ukatili
vinapo tokea katika jamii
"Tumekuja hapa Haubi kwaajili kuwezesha masuala ya yote ya
kijinsia lengo ni kuwezesha na kuweka mikakati ya ufumbuzi lakini pia wao
wemeweza pia kuibua na kuibua kero zilizopo katika jamii yao "
Aidha, pia bi Grace
amsema wameibua kero ya Ardhi ambayo haitoshelezi baada ya wakazi wa Kijiji cha Mafai
kutakiwa kupisha maeneo ya pori la akiba la mkungunero na hivyo kupelekea
kuwepo kwa Ukatili wa kiuchumi baada ya kukosa maeneo ya uzalishaji na
kuacha shuguli za uzalishaji mama pekee
Akijibia kero zilizoibuliwa na washiriki wa wa semina Diwani
wa kata ya Haubi, Paul irovya
amekiri kuwepo kwa wa kero hizo katika kata na kusema zipo katika za
utatuzi na kero ya Tasaf amesema kuwepo kwa changamoto kwa msimu huu wa
uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukosa
baadhi ya wombea kwa kutokuchukuwa fomu kisa watakosa sifa ya kupata msaada wa
huduma za TASAF wa
kaya masikini kwasababu watakuwa viongozi wa vyama vya siasa na pia
akizungumzia kero ya maji katika Kijiji cha Ntomoko
chenye chanzo cha mradi
mkubwa wa maji kushindwa kuwanufaisha wenyeji wa kijiji hicho cha Ntomoko na
badaka yake kwenda kuwanufaisha wilaya ya jirani ya Chemba.
"Watu Sasa wanogopa kuchukuwa fomu za kugombea nafasi za uongozi
CCM kisa watakosa sifa ya kupata msaada wa huduma za Tasaf na ukiangalia
kweli mtu anazo sifa za huduma lakini anakwamishwa kwakuwa ni kiongozi wa
chama cha siasa
binafi ningependekeza sheria hi ingaliwe
Kwa upande wa washiriki wa semina wameahidi kwenda kuwa mabalozi katika
vijiji vyao katika masuala ya Ukatili wa jinsia katika jamii yao ili
kurahisisha jamii kuelewa Athari za vitendo vya Ukatili wa kinjinsia.
Comments
Post a Comment