OWM - KVAU.
OFISI ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) imetoa mafunzo ya ujuzi tepe ‘Soft
Skills’ kwa makundi maalum ya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga yenye lengo la kujitambua na kujithmini.
Akizungumza wakati wa
mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika kuanzia leo Jumanne Juni 28,2022 hadi
Juni 30,2022 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi Idara
ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe amezitaja miongoni mwa mada
zitakazofundishwa ni pamoja na kujitambua kama wajasiriamali, ujasiriamali na
masoko.
Mada zingine ni
urasimishaji wa biashara na usimamizi wa fedha, afya ya uzazi na ujinsia,afua
zilizopo kwa ajili ya vijana wenye ulemavu na mama wadogo,afua zilizopo kwa
ajili ya vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
“Vijana hawa pia
watapewa mafunzo kuhusu fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi ngazi ya taifa
na mkoa, fursa za mitaji na huduma kwa wajasiriamali zinazotolewa Wataalamu
kutoka taasisi mbalimbali, stadi za uongozi, taratibu za uundwaji wa
vikundi,uundwaji wa vikundi vya uzalishajimali vya vijana, kubainisha mahitaji
ya vikundi na uandaaji wa andiko mradi”,ameongeza Tweneshe.
Mwisho.
Comments
Post a Comment