Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa ujenzi
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kusogeza huduma kwa wananchi
na kuongeza mapato.
Zuberi White |
Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Dodoma, Zuberi White alipokuwa
akifungua Mkutano wa mwaka wa ALAT Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma mwishoni mwa wiki.
White alisema kuwa walitembelea miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuridhishwa na utekelezaji
wake. “Tumeona wenzetu wanavyotekeleza mradi wa ujenzi wa hoteli ya Dodoma
City, ujenzi wa soko la wazi la Machinga, ujenzi wa Kituo cha Afya Chang’ombe,
ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza, ujenzi wa shule ya sekondari Hombolo
Makulu na ujenzi wa jengo la kitega uchumi Mtumba, kwa kweli wenzetu hawa wapo
vizuri na wamejipanga sawasawa” alisema White.
Alisema kuwa miradi hiyo ni mizuri. Pamoja na kutoa
huduma bora kwa wananchi, miradi hiyo itaongeza mapato ya halmashauri, alisema.
Mkutano wa mwaka wa ALAT Mkoa wa Dodoma ulifanyika
katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukitanguliwa na ziara ya siku moja ya
kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa jijini hapo.
MWISHO
Comments
Post a Comment