Na Munir
Shemweta, WANMM DODDOMA
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline, Mabula amewataka
Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa nchini kuanzisha Clinic za Ardhi kwa
ajili ya kushughulikia changamoto za sekta ya ardhi katika mikoa yao
‘’Mjiwekee
utaratibu mzuri wa kusikiliza changamoto za ardhi katika mikoa yenu kwa
kuanzisha Clinc za ardhi, Mwanza wamekuwa wakifanya hivyo na wamefanikiwa’’
alisema Dkt Mabula
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, mbali na Wizara yake kufanya vizuri kwa baadhi ya
mambo lakini kuna changamoto ya kutokuwa makini kwa watendaji na kutolea
mfano wa barua za malalamiko zinazokwenda kwenye ofisi yake kuwa
zingeweza kushughulikiwa katika mikoa husika.
‘’Changamoto
kubwa hatuko serious, barua za malamimko ya migogoro ya ardhi zinakuja kwa
waziri na mimi nazirudisha kwenu kupata ufumbuzi na huko napata majibu why
msingeshughulikia mpaka zije huku? Ndiyo maana migogoro inakuwa mingi’’ alihoji
Waziri Dkt Mabula.
Waziri
wa Ardhi alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Wakuu wa Taasisi
zilizo chini ya Wizara, Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa na watendaji wa
Makao Makao Makuu mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara yake na Bunge
ambapo kiasi cha shilingi 110,323,474,000 kiliidhinishwa kwa mwaka wa fedha
2022/2023.
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, sehemu kubwa ya migogoro ardhi inachangiwa na kutokuwepo
mipango ya matumizi bora ya ardhi kwenye halmashauri hivyo aliwataka Makamishna
wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kuzikumbusha halmashauri katika mikoa yao kutenga
fedha kwa ajili ya mipango hiyo.
Aidha,
aliwataka pia kuhakikisha pesa ambazo halmashauri zinazokopeshwa kwa ajili ya
miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi zinatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa na ile faida inayopataikana itumike kuboresha sekta ya ardhi.
Kuhusu
urasimishaji makazi holela, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
aliwataka Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuhakikisha makampuni
yaliyoshindwa kukamilisha kazi za urasimishaji yanachukuliwa hatua na kuangalia
namna bora ya kukwamua kazi zilizokwama.
‘’Kama
wao wamekwama kukamilisha kazi za urasimishaji ninyi mnafanyaje? Undeni timu
katika mikoa kwenda wilaya moja hadi nyingine kulingana na mahitaji, zoezi hili
lina chanagamoto kubwa sana mfano mkoa wa Tabora umefanya vizuriu sana’’
alisema Dkt Mabula.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani
Kikwete alikemea ucheleweshaji hati kwa wamiliki wa ardhi na kueleza kuwa, kama
kuna tatizo linalosababisha mwananchi kutopata hati yake haraka basi aelezwe
badala ya kumuacha mpaka aanze kulalamika.
‘’Kuna
kilio cha wananchi hati kuchukua muda mrefu, nina mfano wa Dar es Salaam kuna
mama mmoja hati yake ilichukua miaka saba na tatizo lake ilikuwa kitambulisho
cha NIDA lakini hakuelezwa hadi akaja kulalamika kwangu, kama lipo tatizo
mhusika aelezwe mapema, maduhuli yanakosekana kutokana na wananchi kutopewa
hati’’ alisema Ridhiwani.
Dkt
Allan Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
alieleza kuwa, ipo changamoto kwa baadhi ya watumishi kufanya kazi bila kufuata
taratibu na taarifa zao hazitolewi na Makamishna wa Ardhi wa Mikoa husika jambo
alilolieleza kuwa, linalosababisha wizara kupata taarifa kupitia vyanzo
vingine,
‘’Kuna
changamoto ya watendaji kufanya kazi bila kufuata taratibu na taarifa
hazipatikani na pale zinapopatikana ni kutoka other sources sasa utendaji wenu
utapimwa pia na jinsi unavyosimamia watendaji wako’’ alisema Dkt Allan Kijazi.
Comments
Post a Comment