Na Mwandishi
Wetu, Dodoma.
Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira imewataka wafanyabiashara wa Soko la Majengo
jijini Dodoma kuyaweka mazingira ya kufanyia biashara katika hali ya usafi ili wateja wanapo kwenda kununua bidhaa
ikiwemo vyakula wakute mazingira ambayo ni safi na salama.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Marry Maganga wakati akizungumza na wafanyabishara wa soko hilo mara baada ya
kufanya ziara ya kikazi kwaajili ya kujionea jitihada za wadau katika usafi wa
mazingira.
‘’Mazingira ni
afya kwa hiyo mjitahidi kuyaweka katika
hali ya usafi ukizingatia kwamba chakula kinauzwa hapa . Sasa mtu anapokuja kununua bidhaa ya
chakula anategemea aikute kwenye mazingira ambayo ni safi.’’ Maganga
‘’Mjitahidi
kuzingatia usafi, mnajitahidi sana pamoja na mazingira kuwa madogo mnajitahidi
kadiri ya uwezo wenu. Basi muongeze nguvu.'' ameongeza Maganga
Kwa upande wa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Ramadhan Kailima amewahimiza kufanya
mikutano ya kila mwezi ambayo itakuwa na ajenda ya mazingira itakayo saidia
kuboresha mazingira ya usafi katika soko hilo.
‘’Tunapongeza
uongozi wa soko namna ambavyo imejipanga . Na niwaombe wafanya biashara wote
tuzingatie usafi bila kufanya usafi hatuwezi kufanya jambo lolote.’’ amesema Kailima
Ziara hiyo ni
sehemu ya Wiki ya Mazingira ambapo kilele chake kitakuwa Juni 5,2022.
Comments
Post a Comment