SENSA YA MAJARIBIO ILIFANIKIWA DODOMA

Na. Theresia Francis, DODOMA

Mratibu wa Sensa ya watu na makazi wa Wilaya ya Dodoma, Calister Makacha ameelezea mafanikio ya Sensa ya majaribio iliyofanyika Septemba, 2021 Kata ya Dodoma Makulu ikihusisha mitaa miwili ya Msangalale Mashariki na Msangalale Magharibi kuwa imeboresha mifumo ya Sensa na kuondoa vikwanzo.

Mratibu wa Sensa na makazi Wilaya ya Dodoma, Calister Makacha akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani


Mafanikio hayo ya Sensa ya majaribio aliyataja wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

“Zoezi lilikua zuri, muitikio ulikua mkubwa sana. Wananchi walijitokeza na walihesabiwa kwa asilimia miamoja. Hakuna aliyeachwa hata waliokuwa wanaenda kazini, makarani waliwasiliana nao kwa namba za simu na kupanga ratiba itakayowawezesha kuhesabiwa” alisema Makacha.

Akiongelea umuhimu wa zoezi la Sensa ya majaribio, alisema kuwa zoezi hilo limesaidia katika kuboresha Sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, mwaka huu. Maboresho hayo aliyataja kuwa ni kuboresha mifumo na kurekebisha vitu ambavyo vilikuwa ni vikwazo katika zoezi la Sensa ya majaribio. 

“Wakati wa Sensa ya majaribio watu walihesabiwa ndani ya siku tatu lakini Sensa ya mwaka huu itakayofanyika Agosti 23 watahesabiwa kwa siku sita kutokana na ukubwa wa maeneo na wingi wa watu walioongezeka tangu walivyogawa maeneo” alisema Makacha.

Sambamba na hilo, Machaka aliwashauri wananchi wa Wilaya ya Dodoma kuacha mtu mmoja katika kaya ambaye anajua taarifa za watu waliolala kwenye kaya usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti ili kutokukwamisha zoezi la Sensa ya watu na makazi. Alisema kuwa ushauri huo ni muhimu kwa sababu shughuli za uchumi zitaendelea kama kawaida.

 

MWISHO

Comments

Dodoma News
Mwanza City, Mwanza, Tanzania
Dennis G. Harrison, mmiliki mwenza wa Mtandao wa Dodoma News Blog, alizaliwa mkoani Morogoro zaidi ya miaka 40 iliyopita. Dennis ana Taaluma ya Uandishi wa Habari (Proffessional Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Mwaka 2009 alimaliza Shahada ya Uzamili katika Mawasiliano ya Umma, ikijikita katika Menejimenti ya Uhusiano kwa Umma na Matangazo katika chuo cha SAUT. Mwaka 2002, Dennis aliajiriwa katika Shirika la Posta Tanzania, Ofisi kuu ya Mwanza. Mwaka 2009 aliajiriwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Afisa Habari. Akiwa katika ofisi hiyo alifanya kazi kwa juhudu na maarifa na kufanikiwa kuchaguliwa na wafanyakazi wote kuwa mfanya kazi bora. Kufuatia juhudi na utendaji kazi wake, alipanda hadi nafasi ya Afisa Habari Mwandamizi.