Dodoma.
Taasisi ya Jamii Mpya Dodoma imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa
kufanya maboresho ya maslahi ya watumishi kwa kupandisha kiwango cha mshahara
kwa asilimia 23.
Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Taasisi hiyo mkoa wa Dodoma Nurdin Ngapanya wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema mbali na maboresho hayo amepandisha pia kiwango cha mafao kwa mkupuo kwa
wastaafu kufikia asilimia 33 kwa watumishi na sekta binafsi.
'' Maboresho haya
yanakwenda kumgusa kila mtanzania na hatimaye kuleta ustawi wa
jamii.’’ amesema Ngapanya
Wakati huo huo, Ngapanya amewahimiza watanzania kote nchini kujitokeza
kwa wingi kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalo tarajiwa
kufanyika mwezi Agosti,2022.
‘’Kila familia iwe na mabalozi wa Sensa ya Watu na Makazi
tuhimizane sisi kwa sisi majirani na jamii zinazo tuzunguka twendeni tushiriki
kikamilifu kwenye zoezi hili.’’ amesisitiza Ngapanya
‘’Tusije tukapoteza fursa hii adhimu ambayo haitokei
tena mpaka ipite miaka 10. Sisi
tumejipanga kupita kata kwa kata ,mtaa kwa mtaa nchi nzima kuhamasisha kushiriki
zoezi la Sensa ya Watu na Makazi. Tunaomba pia makundi na taasisi nyingine
tuungane na serikali yetu kuhamasisha zoezi la Sensa.’’ amehimiza Ngapanya
Mwisho
Comments
Post a Comment