OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKANUSHA ORODHA INAYOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU KUTOKA KWA NAFASI ZA KAZI KWA MAKARANI
Na. Rhoda Simba, DODOMA
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha taarifa zinazosambaa Katika
mitandao ya kijamii kuhusu Kutoka kwa orodha ya majina kwa nafasi za kazi kwa
makarani na wasimamizi wa sensa ya watu na makazi.
![]() |
Dkt. Albina Chuwa |
Taarifa hiyo imetolewa Leo Mei 27 jijini hapa na Mtakwimu Mkuu wa
Serikali, Dkt. Albina
Chuwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema taarifa hiyo
siyo rasmi kwa watanzania waliyo omba nafasi za ukarani na usimamizi wa Sensa
Katika maeneo wanayoishi.
"Kwenye Taarifa inayofanana na hii ambayo pia sio rasmi watu hawa
ambao hawana nia nzuri kwa Serikali na watanzania kwa ujumla wamekwenda mbali
na kutamka tarehe ya usahili kuwa ni tarehe 29 Mei 2022, napenda ifahamike
kwamba mchakato wa ajira za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa Bado
unaendelea Katika ngazi ya kata shehia na Halmshauri zote" amesema Dkt. Chuwa.
Amesema zoezi la uchambuzi wa maombi kwa waombaji wote linatarajiwa
kuanza tarehe 02 Juni 2022 kwenye Kila kata au shehia husika baada ya
kukamilika kwa mafunzo ya maafisa watakaohusika kufanya usahili.
"Mchakato wa ajira za makarani na wasimamizi wa sensa linakwenda
vizuri kulingana na ratiba ya sensa" amesema Dkt. Chuwa.
Hata hivyoo Dkt. Chuwa
amewataka wananchi kwamba taarifa yoyote kuhusu mwenendo wa maandalizi ya sensa
ya watu na makazi sensa ya majengo na sensa ya anwani za makazi ikiwemo ajira
za Muda zitatolewa na Serikali kupitia vyombo vya habari.
Mwisho
Comments
Post a Comment