Na.
Theresia Francis, DODOMA
MKURUGENZI
wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wa
Tanzania na kutoa shilingi bilioni 2.5 za umaliziaji wa Soko la wazi la
Machinga.
Joseph Mafuru |
Pongezi
hizo alizitoa leo katika hafla fupi ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha maslahi ya watumishi katika ukumbi wa
mikutano wa PSSSF jijini hapa.
Mkurugenzi
Mafuru alisema kuwa Rais Samia toka akabidhiwe nchi ameweza kuimarisha
miundombinu kwa kiasi kikubwa na kuboresha maslahi ya watumishi. Maboresho hayo
yanapelekea ufanisi wa kazi kwa watumishi wa umma kuongezeka. “Baada ya Rais
kutangaza ongezeko la asilimia 23.3 kwenye mishahara yao. Watumishi sasa
wanafanya kazi kwa bidii, ukienda kwenye kata unawakuta, kwenye mitaa unawakuta
wanasimamia miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa. Morali ya watumishi imerudi
juu” alisema Mafuru.
Mkurugenzi
huyo aliwashauri watumishi kuendana na kasi ya maboresho ya maslahi ya
watumishi wa umma aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan. “Kuanzia Julai,
mishahara ya watumishi inaenda kubadilika, sitegemei kufika Agosti au Septemba
kuona wananchi wakiendelea kupata huduma ileile kama ya miaka miwili iliyopita.
Ni deni kwetu watumishi kupambana kuonesha kuna kitu kimeongezeka kwenye
utekelezaji wa majukumu yetu” alisema.
Aidha,
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza
kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ili kumalizia mradi wa Soko la wazi la Machinga.
Alisema kuwa halmashauri yake ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 4.9 kwa ajili
ya awamu ya kwanza ya ujenzi huo.
MWISHO
Comments
Post a Comment